Maandalizi ya Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa EAC yaanza Arusha

Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Mashauriano ya Kibajeti unafanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 3 hadi 7 Mei 2021.
Sehemu ya Wajumbe wa kikao cha Wataalam wakiwa wamesimama kabla ya kuanza kikao chao ili kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyefariki dunia mwezi Machi 2021. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).Kamishna wa Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. William Mhoja (kushoto) akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya wataalam ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Arusha tarehe 7 Mei 2021. Mkutano wa Wataalam unafanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Mei 2021 na kufuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu tarehe 6 Mei 2021. Kulia ni Bw. James Msina, Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Fedha na Mipango.
Bw. James Msina, Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kikanda kutoka Wizara ya Fedha na Mipango akichangia jambo wakati wa kikao cha wataalam wanaoandaa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkuu wa Idara inayoshughulikia masuala ya Fedha katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Pantaleo Kessy (kushoto) akichangia jambo wakati wa kikao cha wataalam.
Ujumbe kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Uganda wakishiriki mkutano wa ngazi ya wataalam ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Arusha tarehe 7 Mei 202.
Mjumbe kutoka Burundi akishiriki mkutano wa wataalam.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Elias Bagumhe akishauriana jambo na mjumbe kutoka Tanzania wakati wa kikao cha wataalam.
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea.
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania kwenye kikao hicho
Ujumbe ulioshiriki kikao cha waatalam.

Mkutano huo ambao umeitishwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, umetanguliwa na kikao cha Ngazi ya Wataalam kutoka Sekta za Fedha na Uchumi unaofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Mei 2021 na kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu tarehe 6 Mei 2021 kabla ya kuhitimishwa na Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri mnamo tarehe 7 Mei 2021.

Mkutano huo wa 12 pamoja na mambo mengine una lengo la kupokea na kujadili taarifa za Kamati zinazoshughulikia masuala ya Fedha pamoja na kufanya mashauriano ya awali ya Bajeti ya Mawaziri wa Fedha na masuala ya Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Vilevile, utapokea Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio mbalimbali yaliyofikiwa wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza hilo la Kisekta.

Ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha ngazi ya Wataalam unaongozwa na Bw. William Mhoja, Kamishna wa Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news