MAJALIWA ATAKA HATUA ZAIDI ZICHUKULIWE KWA WANAOHUSIKA NA MFUMO WA LUKU

Na Diramakini (diramakini@gmail.com)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amemuagiza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani asiishie kuwasimamisha kwa siku kumi tu meneja wa TEHAMA na wasaidizi wake, bali wakae pembeni hadi hapo uchunguzi zaidi utakapokamilika.

Ametoa agizo hilo leo Mei 20, 2021 alipozungumza na Menejementi na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwenye makao makuu ya zamani Shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO kwenye Makao Makuu ya zamani ya Shirika hilo Ubungo jijini Dar es salaam, Mei 20, 2021. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

“Lazima tufundishane kuwa makini, kila siku lazima tukague vifaa vyetu ili huduma ipatikane muda wote. Hakuna kuwasimamisha kwa siku 10, wakae pembeni hadi timu inayochunguza itakapotoa matokeo. Inawezekana sio wao tu, Waziri endelea na uchunguzi”

Aidha, Waziri Mkuu ameliagiza shirika hilo kuhakikisha wanakuwa na mfumo wa dharura ‘backup’ utakaotumika pindi kunapotokea changamoto za kimfumo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakati alipowasili kwenye Makao Mkuu ya zamani ya Shirika hilo, Ubungo jijini Dar es salaam, Mei 20, 2021. Kushoto ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani.  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO kwenye Makao Makuu ya zamani ya Shirika hilo Ubungo jijini Dar es salaam, Mei 20, 2021. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO kwenye Makao Makuu ya zamani ya Shirika hilo Ubungo jijini Dar es salaam, Mei 20, 2021. Kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Baadhi ya Viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Makao Makuu ya zamani ya Shirika hilo jijini Dar es salaam, Mei 20, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 
“Mmetengeneza usumbufu mkubwa sana, mlijua lazima kuwe na backup lakini hakuna, toka pale tulipoanza kutoa huduma mpaka leo kwanini hakuna backup, hilo ni jukumu lenu,”amesema.

Amesema kuwa Serikali inataka kuona huduma hii inapatikana muda wote. “Jitihada za Serikali kuimarisha vyanzo vya umeme zina lengo la kuhakikisha tunapata umeme mwingi na wa gharama nafuu”.

Naye, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema hakuridhishwa na watendaji wanaosimamia mfumo na amewaomba radhi watanzania kwa usumbufu uliojitokeza.

Pia amesema amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Nishati aunde kikosi kazi maalum kwa ajili kuupitia upya mfumo

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news