Mbunge wa Jimbo la Konde afariki

Na Diramakini (diramakini@gmail.com)

CHAMA cha ACT Wazalendo kimempoteza Mbunge wake kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Khatib Said Haji kutoka Jimbo la Konde kisiwani Pemba.

Mheshimiwa Haji ni miongoni mwa wabunge ambao hivi karibuni walizua gumzo bungeni baada ya kudai kuwa, mahabusu wa Uamsho wanamliza.

Kutokana na uwepo wa mahabusu hao kwa muda mrefu gerezani Tanzania Bara aliomba Serikali ifanye uamuzi wa busara ili kuona wanapewa haki ya kuachiwa huru.

Kifo cha Mheshimiwa Haji kimethibitishwa na Katibu Idara ya Bunge Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa, Hamad Yussuf leo Mei 20, 2021.

"Nasikitika kuwatangazia Kifo Cha Mhe Khatib Said Haji Mbunge wa Jimbo la Konde, ambaye umauti umemfika akiwa anapatiwa Matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Alfajiri ya leo, mipango ya mazishi inaendelea na tutajulishwa baadae kidogo.
 
"Kwa Niaba ya Idara ya Bunge, Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa natoa pole kwa Kiongozi wa Chama na Viongozi wengine wote Familia, na Wananchi wa Jimbo la Konde, Allah Amsamehe makosa yake, ampe kauli thabiti ampe pepo ya Firdaus na sisi atujaalie mwisho mwema Aamin,"ameeleza Yussuf.
 
AKIWA CUF
 
Marehemu kabla ya kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo wakati akiwa Mbunge wa Konde kupitia Chama cha Wananchi (CUF) katika Bunge lililoishia mwaka 2020 anakumbukwa kwa hoja yake ya kuiomba Serikali kumchukulia hatua Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Salama Aboud Talib aliyekataa kukaa karantini na kusababisha maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) kwa watu wawili kwenye familia yake.

Akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 alisema , matokeo ya hilo nyumbani kwake kuna watu wawili amewaambukiza na huko hospitali haijulikani matokeo yake nini.

“Ndani ya siku tatu ameng’ang’ana kukaa hospitali ya Mnazi Mmoja matokeo yake akatolewa kwa nguvu baada ya kuona jambo hili limekuwa kubwa sana. Baada ya malalamiko makubwa ndio alikubali kuwekwa kwenye karantini,”aLIsema Haji wakati wa uhai wake.

ALIsema alifanya hivyo kwa sababu ya kiburi cha madaraka yake na kumpongeza makamu wa pilli wa Rais Zanzibar wakati huo kabla ya Serikali ya Awamu ya Nane kwa kukubali kukaa karantini alipotoka nje ya nchi bila kulazimishwa.

“Huu ndio utu, huu ndio ubinadamu leo waziri huyu ni nani anayekataa uamuzi wa Serikali hata uamuzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Hatuwezi kumchekea mtu mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu ni waziri ulichukulie hatua haraka. Leo hii baada ya kiburi kingine kuna mtu mwingine ni daktari anaitwa Hafidh hadi leo ameng'ang'ana pale Hospitali ya Mnazi mmoja kwa sababu ana unasaba wa kiukubwa.

“Uheshimiwa wake ni kwa sababu ana uhai anapumua dakika moja akifumba macho anakuwa marehemu. Taharuki iliyopo pale Mnazi mmoja baada ya matukio hayo ni kubwa. Nataka mheshimiwa ufuatilie kama huyu daktari bado yupo,”alisema.

Mheshimiwa Khatibu aliwahi kuwa Mbunge wa Konde kupitia Chama cha Wananchi CUF mwaka 2010 hadi 2020. Pia alishawahi kushika nafasi ya Waziri wa Kilimo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1984 hadi 1987.

Katika Bunge hili la 12, Khatib amekuwa Mbunge wa tatu kufariki tangu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Januari 21, 2021 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla alifariki dunia na Februari 12, 2021 Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Atashata Nditiye alifariki dunia baada ya kupata ajali ya gari mkoani Dodoma.


WASIFU WA MHESHIMIWA KHATIB SAID HAJI KABLA YA KUJIUNGA ACT WAZALENDO UCHAGUZI WA MWAKA 2020.

Hon. Khatib Said Haji

Member Type : Constituent Member

Constituent : Konde

Date of Birth : 1962-07-31

Education History :

School Name/Location Course/Degree/Award From To Level
Konde Secondary School - 0 0 Secondary School
Utaani Secondary School CSEE 0 0 Secondary School
Micheweni Primary School CPEE 0 0 Primary School

Employment History :

Company/Institution Position From To
Ministry of Agriculture (SMZ) Pay Master/Accounts 1984 1987

Political Experience :

Political Party Position From To
Economic Affairs, industries and Trade Committee Member of Committee 2010 2015
Parliament of Tanzania Member of Parliament 2015 2020
Parliament of Tanzania Member of Parliament 2010 2015
Civic United Front (CUF) Member of District Committee 1995 1995
Industries, Trade and Enviroment CommitteeMember20152018

Post a Comment

0 Comments