Kamati Kuu ya CCM chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan imemteua Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Dkt. Lazaro Komba, kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma.
Uamuzi huo umefanyika Jumapili, Januari 25, 2026, katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Zanzibar.
Uchaguzi mdogo wa ubunge wa Peramiho utafanyika Februari 26, 2026, kujaza nafasi iliyoachwa wazi na marehemu Jenista Mhagama aliyefariki Desemba 11, 2025.
Katika kura za maoni za CCM zilizofanyika Januari 22, 2025, Dkt.Komba alipata kura 213 kati ya 9,167 na kushika nafasi ya tano kati ya watia nia 27. Victor Mhagama aliongoza kwa kura 3,040.


























