Rais Dkt.Mwinyi afanya ziara eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari ya Magapwani

Na Diramakini (diramakini@gmail.com)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanya ziara katika eneo linalotarajiwa kujengwa bandari mpya ya Magapwani na kueleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa maamuzi yenye tija kwa ajili ya muendelezo wa eneo hilo.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo mara baada ya kufanya ziara ya kulitembelea eneo linalotarajiwa kujengwa bandari mpya ya Mangapwani, Wizaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo pia, alitembelea miradi ambayo imeanza kabla ya ujenzi huo mpya.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutaka ufafanuzi, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud,wakati wa ziara yake kutembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari ya Kisasa katika eneo la Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja, akiwa katika eneo la Mradi wa Island Petroleum Group.tayari limejengwa matangi ya mafuta.

Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali itakuja na maamuzi yenye tija ambayo yatasaidia kwa pande sote mbili ikiwemo upande wa wawekezaji ambao walianza kuekeza kwa muda mrefu katika eneo hilo pamoja na kwa upande wa Serikali kwa ujumla huku akiwataka wawekezaji hao kuwa na subira.Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali imeridhishwa na ukubwa wa eneo pamoja na hatua ya awali iliyofikiwa na kuelez ajambo kubwa lililompelekea kufanya ziara hiyo hivi leo ikiwa ni kwenda kujiridhisha na kulielewa vyema eneo hilo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar.(hawapo pichani) baada ya kumaliza ziara yake kutembelea eneo la Ujenzi wa Bandari ya Kisasa Mwangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliwasisitiza wawekezaji hao kuwa na subira huku akisema kwamba atahakikisha jambo hilo linakwenda kwa haraka na ameahidi kukaa na wahusika mapema iwezekanavyo kwa azma hiyo hiyo ya kuharakisha mradi huo.Alitumia fusra hiyo kutoa shukurani kwa wananchi wa eneo hilo kwa utayari wao waliouonesha kwa kuruhusu maendeleo kwa kushirikiana na Serikali yao kwa kuupisha mradi huo mkubwa wa bandari.

Pia, Rais Dk. Mwinyi alitoa shukurani kwa wataalamu pamoja na washauri elekezi kwa kumaliza hatua ya mwanzo kwa kipindi cha miezi mitatu huku akieleza hatua zitakazofuata hivi sasa sambamba na maamuzi yatakayochukuliwa.Aliongeza kwamba Serikali inafanya juhudi hizo kwa kuamini kwamba hivi sasa Bandari ya Malindi haikidhi haja tena na ndio maana imeamua kuanzisha mradi huo mkubwa wa Bandari ya Mangapwani kwa maendeleo ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutaka ufafanuzi, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud,wakati wa ziara yake kutembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Bandari ya Kisasa katika eneo la Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja, akiwa katika eneo la Mradi wa Island Petroleum Group.tayari limejengwa matangi ya mafuta. (PICHA ZOTE NA IKULU).

Katika ziara yake hiyo, Rais Dk. Mwinyi alitembelea eneo la mradi wa Chelezo, Mradi wa Islana Petroleum, Mradi wa Salama International Company na eneo la Mradi wa TP Invetment Depot na kupata maelezo kutoka kwa viongozi wa Serikali na wawekezaji.Akiwa katika eneo hilo, Mapema alipata maelezo ya mradi huo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Amour Hamil Bakari ambaye alimueleza namna ya michoro ya mradi huo zinavyoelekeza huku Katibu Tawala wa Mkoa huo wa Kaskazini Unguja Makame Machano Haji akieleza namna walivyoshirikiana na mshauri elekezi kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Nao wawekezaji wa eneo hilo ambao walianza kuekeza miradi yao kabla ya kuanzishwa kwa mradi huo mkubwa kwa nyakati tofauti walimueleza Rais Dk. Mwinyi hatua walizofikia katika miradi yao huku wakionesha utayari wao wa kuendelea kushirikiana na Serikali.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Ndg. Amour Hamil Bakari,akitowa maelezo ya michoro ya Ramani ya eneo la Ujenzi wa Bandari ya Kisasa katika eneo la Mwangapwani Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza CEO wa Kampuni ya United Petroleum Ndg.Collins Chemngorem, akiwa katika ziara yake katika eneo linalotarajiwa ujenzi wa Bandari ya Kisasa Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja, na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud na (kulia kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Rahma Kassim Ali.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndg. Makame Machano Haji akitowa maelezo ya eneo la Ujenzi wa Bandari ya Kisasa Mwangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja wakati wa ziara yake kutembelea eneo hilo na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud na (kulia kwa Rais) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe. Rahma Kassim Ali

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud alitumia fursa hiyo kumkaribisha Rais Dk. Mwinyi katika Mkoa huo pamoja na kueleza hatua zilizofikiwa na mradi huo kwa mashirikiano na wataalamu wa Wizara husika wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Rahma Kassim Ali.

Mnamo Mei 07, 2021 Rais Dk. Mwinyi alipokea Mpango wa ujenzi wa Bandari ya kisasa ya Mangapwani kutoka Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman (OIA), chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Sheikh Mohammed Al Tooq ambapo mradi huo unahusisha maeneo makuu matatu, ikiwemo ujenzi wa Bandari mbali mbali, mji wa kisasa wa makaazi pamoja na Mpango wa kuiendeleza Bandari ya Malindi ili iweze kutumika kama Bandari ya utalii.

Post a Comment

0 Comments