TUME YA UTUMISHI WA UMMA KUTOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA KADCO

Tume ya Utumishi wa Umma inatarajia kutoa mafunzo kwa Watumishi wa Kampuni ya Uendelezaji wa Kiwanja cha Ndege Kilimanjaro (KADCO) mkoani Kilimanjaro.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bwana Nyakimura Muhoji. (Picha na Tume ya Utumishi wa Umma).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bwana Nyakimura Muhoji amesema kuwa mafunzo haya yameandaliwa na KADCO kwa lengo la kuwajengea uwezo Watumishi wa KADCO.

Ni kuhusu Utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298 na Usimamizi wa Utendaji Kazi kupitia Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji kazi (OPRAS), kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayosimamia masuala ya Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma.

Mafunzo haya ya wiki mbili yatafanyika kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 10 Mei, 2021 na yatafunguliwa Rasmi na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa George D. Yambesi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana na yatahitimishwa tarehe 24 Mei, 2021.

Bwana Muhoji amesema, Tume inatekeleza jukumu hili kwa mujibu wa Kifungu cha 10 (1) ( C) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura 298.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news