UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 16/05/2021

Mikoa ya Kagera na Mara: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Geita, Mwanza na Simiyu: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku 16/05/2021 umeletwa na mchambuzi Tabu Kwedilima.

Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Kilimanjaro, Arusha , Manyara, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, pamoja na (Visiwa vya Unguja na Pemba): Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Njombe, Iringa, Songwe, Dodoma, Singida, Tabora na Katavi, Ruvuma, Kigoma, Shinyanga, pamoja na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

KIWANGO CHA JUU ZAIDI CHA JOTO NI NYUZI JOTO 32 ( 32°C ) KATIKA MIJI YA MTWARA NA TANGA.

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kusini kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa Kiasi.

Matarajio kwa siku ya Jumanne tarehe 18/05/2021: Mabadiliko Kidogo.

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 16/05/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Post a Comment

0 Comments