Waziri Ndungulile aahidi neema kwa wakulima kupitia simu, afurahishwa na ubunifu wa TARI

Waziri wa Mawasiliano na  Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndungulile amesema kuwa wizara yake itahakikisha  inaimarisha mitandao ya simu hadi vijijini ili kuwawezesha wakulima  kupata habari za kutosha na elimu za mazao mbalimbali  zinazotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

Waziri Ndungulile ameyasema hayo wakati akizungumza na watafiti wa kilimo pamoja na watumishi wa taasisi hiyo leo Mei 10,2021 katika viwanja wa Jamhuri yanapoendelea maonesho ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ambapo taasisi inashiriki kuonesha namna teknolojia inavyotumika kuchochea mapinduzi ya kilimo nchini.

Dkt. Ndungulile amesema wizara yake inatambua mchango mkubwa unaotolewa na watafiti wa kilimo katika kuwasaidia wakulima ambapo amesema watahakikisha wanaboresha teknolojia katika sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wakulima kupata habari za kiutafiti kupitia mitandao mbalimbali  ya kijamii. (Picha zote na Junior Mwemezi -Idara ya Habari na Mawasiliono  TARI makao makuu).

Post a Comment

0 Comments