Waziri Ummy Mwalimu atangaza ajira 6,649 za walimu, afya 2,726

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Ummy Mwalimu ametangaza ajira za walimu 6,649 na watumishi wa Afya 2,726 ambao wametakiwa kutuma maombi kuanzia leo hadi Mei 23,2021, ANARIPOTI MWANDISHI DIRAMAKINI.

Mfumo uko wazi kwa waombaji wa ajira za Elimu na Afya bofya hapo chini

https://ajira.tamisemi.go.tz/#/authentication/login

Waziri Ummy amesema ajira hizo ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, la kuajiri wafanyakazi zaidi ya elfu sita.

Akizungumza jijini Dodoma leo Mhe.Ummy amesema ajira hizo zinakwenda kuziba mapengo ya wafanyakazi waliostaafu, waliofariki na wengine kuacha kazi hivyo ajira hizo ni za watanzania na kwa wale watakaokidhi vigezo watapatiwa ajira kwa haraka ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Ameongeza kuwa ajira zitatolewa kwa haki na waombaji wasitoe fedha yeyote ili kupata ajira kwakuwa baadhi ya watu wanaweza kutumia vibaya fursa hiyo.

Post a Comment

0 Comments