Ajali ya treni yaua 40, yajeruhi 120

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Zaidi ya watu 40 wanahofiwa kufariki huku 120 wakijeruhiwa vibaya katika ajali ya treni iliyotokea Kusini mwa mji wa Dharki nchi Pakistani.

Ajali hiyo imehusisha treni mbili za mwendo kasi ambapo kwa sasa vikosi vya uokoaji vinaendelea kushirikiana kwa ajili ya kutafuta watu waliokuwemo katika treni hizo.

Tukio hilo limetoke mapema leo Juni 7, 2021 katika mji huo ambao upo zaidi ya kilomita 440 kutoka mji Mkuu wa Serikali wa Karachi.
Wanajeshi wakishirikiana na vikosi vya uokoaji kuondoa miili ya watu ambao wamekufa katika ajali ya treni Wilaya ya Ghotki iliyopo Kusini mwa Pakistan leo. (Picha na Stringer/Reuters/Diramakini Blog).

Kwa mujibu wa taarifa za awali, kuna idadi kubwa ya watu ambao bado wamekwama kwenye mabaki ya mabehewa karibu na mji wa Daharki, jimbo la Sindh.

DIRAMAKINI BLOG imekariri moja ya taarifa za wito kutoka kwa waokoaji ambao wameomba haraka kupelekewa vifaa mahsusi kuwasaidia kukata vyuma ili kuwatoa watu ambao wapo ndani ya mabehewa.

Afisa mwandamizi wa polisi wa mji wa Daharki, Umar Tufail amethibitisha idadi ya waliopoteza maisha.

Aidha, picha zilizosambaa kwenye vyombo vya habari zinaonesha miili ikiwa imelazwa chini ikifunikwa sanda nyeupe.

Waziri Mkuu Imran Khan amesema, ameshtushwa na ajali hiyo, na kuahidi uchunguzi kamili. Jeshi limetumwa kusaidia juhudi za uokozi. Ajali za treni hutokea mara kwa mara nchini Pakistan, ambayo ilirithi maelfu ya kilomita ya njia za reli kutoka kwa mkoloni wake wa Uingereza.

Post a Comment

0 Comments