Joshua Nassari, Mashinji wateuliwa wakuu wa Wilaya

Na Mwandishi Diramakini

Katika uteuzi huo, Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Vicent Mashinji kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Pia amemteua Joshua Samwel Nassari kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Joshua Nassari na Mashinji kabla ya kujiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM) walitokea Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Uteuzi huu umefanyika leo na Wakuu wa Wilaya wateule wataapishwa kuanzia tarehe 21 Juni, 2021 saa nne (4) asubuhi na Wakuu wa Mikoa yao.

Post a Comment

0 Comments