Kahata wa Simba SC arejea nyumbani

Imeelezwa kuwa, kiungo mchezeshaji wa Simba SC raia wa Kenya, Francis Kahata ameshindwa kufikia muafaka mzuri na timu yake katika dau la usajili, hivyo kulazimika kukusanya kila kilicho chake na kurejea nyumbani.
Nyota huyo tayari amemaliza mkataba wake wa miaka miwili ya kukipiga Simba SC aliyojiunga nayo msimu wa 2019/2020 akitokea Gor Mahia ya Kenya kama mchezaji huru.

Kahata hivi karibuni jina lake lilikatwa katika usajili wa Ligi Kuu Bara na nafasi yake kuchukuliwa na Mzimbabwe, Perfect Chikwende aliyejiunga na Simba SC katika usajili wa dirisha dogo msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo Simba imeshindwa kufikia muafaka mzuri wa kumuongezea mkataba baada ya kushindwana katika maslahi kwenye pande hizo mbili.

Post a Comment

0 Comments