KMC FC WAENDELEA KUJIFUA KUWAKABILI DODOMA JIJI JUNI 17

Kikosi cha KMC FC kimeendelea kujifua kuelekea katika michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara iliyosalia kabla ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu 2020/2021 ambapo itakuwa ugenini Juni 17 katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.
KMC FC inajiandaa na mchezo wake muhimu ambao utakuwa dhidi ya Dodoma Jiji na kwamba mipango ya makocha, Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na Habibu Kondo ni kuhakikisha kwamba inafanya vizuri na hivyo kuendelea kusonga mbele kwa michezo mingine iliyosalia.

Aidha Kino Boys hivi sasa imebakiza michezo mitano ambayo kati ya hiyo minne itakuwa nyumbani huku mmoja ambao ni dhidi ya Dodoma Jiji itakuwa ugenini ambapo Timu na uongozi kwa ujumla inaendelea kujipanga ili kuhakikisha kwamba inafanya vizuri na hivyo kumaliza msimu ikiwa kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa Ligi kuu.

Michezo ambayo KMC FC imebakiza kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2020/2021 hivi sasa ni dhidi ya Dodoma jiji, Mtibwa Sugar, JKT Tanzania ,Simba pamoja na Ihefu huku ikiwa imeshacheza michezo 29 na kujikusanyia alama 41 na kuwa kwenye nafasi ya tano ya msimamo wa Ligi Kuu.

Tunaendelea na maandalizi, wachezaji wote wanamorali na hari ya kuhakikisha kwamba kile ambacho wanaelekezwa na makocha wanakifanyia kazi kwenye michezo husika jambo ambalo linawezekana kwakuwa michezo yote licha ya kwamba itakuwa naushindani mkubwa lakini bado ipondani ya uwezo wa KMC FC.

Imetolewa leo Juni 02

Na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mahusiano wa KMC FC

Post a Comment

0 Comments