Kanisa Katoliki latangaza marekebisho kanuni za jinai

Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis ametangaza marekebisho kwenye kanuni za jinai za kanisa hilo.

Miongoni kwa marekebisho hayo ni adhabu dhidi ya mapadri na wengine wanaotumia nguvu, vitisho au kutumia vibaya madaraka kwa kujihusisha katika vitendo vya ngono.
Papa Francis ametangaza uamuzi huo Juni 1,2021 ambapo mapadri wanaotenda makosa hayo dhidi ya watoto na watu wazima wanaweza kutenguliwa, nao watumishi wa kawaida watafukuzwa kazi au walipe faini.

Pia marekebisho hayo yanaeleza kwamba maaskofu na viongozi wengine wa kidini wanaweza kuwajibishwa iwapo watashindwa kufanya uchunguzi kamili ni kuwaadhibu mapadri wanaofanya vitendo viovu.

Hata hivyo, kipengele kipya kinaeleza ni kitendo cha uhalifu kwa mapadri kumuhusisha mtoto kwenye utendaji wa ngono.

Post a Comment

0 Comments