Lengai Ole Sabaya, wenzake wafikishwa mahakamani

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Leo Juni 4, 2021 aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kujibu tuhuma zinazowakabili. 
 
Kabla ya hatua ya leo, Sabaya alikuwa anashikiliwa kwa siku kadhaa na makachero wa Taaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa ajili ya uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya akiwa na wenzake.
 
Lengai Ole Sabaya amefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi akiwa na walinzi wake 6 na baada ya kushuka kwenye magari pamoja na wenzake walitakiwa kuchuchumaa kusubiri taratibu nyingine ambapo baadae walichukuliwa na kupelekwa chumba maalum kabla ya hatua zaidi.
 
Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache zimepita baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumsimamisha kazi mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Taarifa iliyotolewa Alhamisi ya Mei 13, 2021 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa ilieleza kuwa, Sabaya alisimamishwa kazi kuanzia tarehe hiyo.

Rais Samia alichukua uamuzi huo ikiwa mheshimiwa Sabaya amehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka michache tangu alipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli Julai 28, 2018.HABARI KWA KINA ZINAKUJIA HAPA FUATILIA DIRAMAKINI BLOG

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news