MAJALIWA AWAAGIZA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI KUFUFUA MADARASA YA MEMKWA

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanafufua madarasa kwa ajili ya Mpango wa Elimu ya Msingi kwa walioikosa (MEMKWA) ili kusaidia kupunguza ongezeko la watu wazima wasiojua kusoma na kuandika.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wakionyesha vitabu baada ya Waziri Mkuu kufungua kongamano la kimataifa la kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania kwenye ukumbi wa maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Juni 9, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Ametoa agizo hilo leo Juni 9, 2021 wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania.

“Naagiza madarasa ya MEMKWA yahuishwe. Wakuu wa Mikoa na Wilaya suala la elimu ya watu wazima liwe sehemu ya ajenda zenu mnapofanya ziara. Fuatilieni kuiona elimu ya watu wazima inahuishwa ili kupunguza na ikiwezekana kuondoa kabisa tatizo la kutokujua kusoma na kuandika,"amesema.

Aidha, amewataka watumie madarasa hayo kuwezesha watu wazima wapate stadi mbalimbali pamoja na stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha tuzo aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kutokana na mchango wake katika kufanikisha kongamano la Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania baada ya kufungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Juni 9, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo Balozi Nicholas Kuhanga ambaye pia Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Mstaafu wakati Waziri Mkuu alipofungua Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania kwenye ukumbi wa maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Juni 9, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu amesema kuwa pamoja na kutekeleza majukumu mengine, Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima iendelee kutekeleza kikamilifu jukumu lake la msingi la utoaji wa elimu ya watu wazima hadi katika ngazi ya wilaya

“Andaeni mkakati wa kusimamia utoaji mafunzo ya stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watu wazima badala ya kutoa astashahada, shahada na stashada tu. Idadi wa Watu wazima wasiojua kusoma imeongezeka hamna jinsi ya kukwepa jukumu lenu hili. Jipangeni upya ninafahamu fika Elimu ya Watu Wazima ni zaidi ya KKK”.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka wataalam na wanataaluma wa Elimu ya Watu Wazima kutoa ushauri kuhusu namna ya kuboresha Vyuo vya kati vinavyotoa mafunzo mbalimbali ili kuzalisha wahitimu mahiri wanaohitajika katika viwanda na taasisi nyingine.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo (wa pili kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa William Anangisye (kulia) wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufungua kongamano la kimataifa la miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania, Juni 9, 2021. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu). Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kimataifa la kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua kongamano hilo kwenye ukumbi wa maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Juni 9, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Kimataifa la Kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania kwenye ukumbi wa maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Juni 9, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua Kongamano la Kimataifa la kuadhimisha Miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania kwenye ukumbi wa maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Juni 9, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Akizungumza wakati alipotembelea mabanda katika maadhimisho hayo, Waziri Mkuu ameitaka Taasisi ya Elimu ya Watu wazima kuwatumia maafisa elimu ya watu wazima waliopo kwenye Halmashauri kwa kuwapelekea programu za elimu ya watu wazima ili wazitekeleze bila kujali kama wako kwenye mamlaka gani.

Naye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi katika kutoa mafunzo ya elimu kwa watu wazima wanaohitaji kujiendeleza kitaaluma na kitaalam.

Amesema kuwa lengo ni kuhakikisha wanawasaidia kujishughulisha kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali na hatimaye kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news