Naibu Waziri wa Mafuta wa Iran, Mohammad Sadegh Azimifar, amesema nchi hiyo inalenga kurejesha kati ya asilimia 70 hadi 80 ya uwezo wake wa kusafisha na kusambaza mafuta ndani ya miezi miwili ijayo.







Akizungumza na shirika la habari la SNN, Azimifar alisema miundombinu ya mafuta ikiwemo viwanda vya kusafisha, njia za usafirishaji, maghala ya mafuta na vituo vya kujaza mafuta ya ndege imeharibiwa kufuatia mashambulizi yaliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Alisema timu maalum zimepelekwa kuondoa vifusi na kubadilisha vifaa vilivyoharibiwa, ikiwemo katika kiwanda cha kusafisha mafuta kilichopo Kisiwa cha Lavan.
Kwa mujibu wa mpango huo, sehemu ya uzalishaji katika kiwanda hicho inatarajiwa kuanza tena ndani ya siku 10 zijazo, ikiwa ni hatua ya awali ya kurejesha uzalishaji wa mafuta nchini humo.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo












