Mizaha ya madereva ilivyozima maisha ya watu tisa, kujeruhi 24

Na Mwandishi Diramakini

Saa chache baada ya ajali iliyoua watu tisa mkoani Morogoro, miongoni mwa abiria aliyenusurika katika ajali hiyo amefunguka mengi.
Ajali hiyo ya usiku wa kuhamkia leo Juni 22, 2021 imehusisha lori mali ya Kampuni ya Dangote na basi dogo aina ya Coaster.

Frank Ramsoni amesema, gari hiyo ya Coaster ilikuwa inatoka Dar es Salaam kuelekea Mbeya walipofika njiani dereva aliweka mashada kwenye gari hilo kama ishara imebeba maiti ili kupata wepesi wa kufanya safari ambapo baada ya kufika eneo la Kingulwira Manispaa ya Morogoro gari hiyo ilisimamishwa na askari.

Hivyo alishuka kwa ajili ya kwenda kumsikiliza.

Amesema, wakati dereva huyo akiwa na trafiki, msaidizi wake aliyekuwa kushoto aliondoa basi hilo bila idhini ya dereva wake.

Pia abiria huyo amesema, dereva huyo alianza kuendesha basi hilo kwa mwenzdo kasi huku mkono mmoja ukizungumza na simu.

Kwa mujibu wa abiria huyo mawasiliano ya dereva huyo yalikuwa ni kati yake na dereva mwingine waliyemuacha akizungumza na trafiki na kwamba inaelekea alikuwa akimsisitiza asimame, lakini hakufanya hivyo hadi basi hilo lilipogongana uso kwa uso na lori.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim ameonya huku akikemea madereva wa magari kuacha kuweka maua kwenye magari ili ionekane wanakwenda msibani lengo likiwa kukwepa kusimamishwa na askari wa usalama barabarani.

Amesema, gari dogo la abiria aina ya Coaster lilikuwa na mashada ya maua wakiashiria kuwa walikuwa wanapeleka maiti ili askari wasiwakamate.

"Nawaonya madereva kuacha tabia kama hii, tumejipanga vizuri kuhakikisha udanganyifu kama huo hautokei tena,” amrsema Kamanda huyo.

Kamanda amesema, ajali hiyo imehusisha magari matatu na kusababisha vifo vya watu tisa na majeruhi 24 ambapo watu watano walifariki hapo hapo.

Amesema, chanzo cha ajali hiyo ni gari aina ya Toyota Coaster lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya likiendeshwa na Minde kutaka kulipita gari jingine aina ya Toyota Cresta lililokuwa likiendeshwa na Emmanuel Sembuche bila kuchukua tahadhari.

Amesema, gari hilo liliigonga Cresta na kupoteza mwelekeo na kukutana uso kwa uso na lori hilo.

Pia Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kesy Ngalawa amesema kati ya hao majeruhi watano wapo chumba maalum cha uangalizi (ICU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here