Bajeti ya 2021/2022 yapitishwa rasmi bungeni

Na Mwandishi Diramakini

Leo Juni 22, 2021 Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepitisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2021/2022.

Bajeti hiyo imepitishwa na wabunge hao Bungeni jijini Dodoma ambapo kabla ya kupigiwa kura na wabunge kwa ajili ya kupitishwa, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Nchemba amehitimisha kwa kutolea ufafanuzi hoja za wabunge walizozitoa kwenye michango yao.

Kupitia bajeti hiyo Serikali imeongeza mabilioni ya fedha katika sekta za afya, elimu, barabara na maji ili kuongeza tija na ufanisi kwenye maeneo hayo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akijibu hoja wakati wa kuhitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya Sh. trilioni 36.66 kabla ya Bunge kuidhinisha Bajeti hiyo Bungeni jijini Dodoma.

Akizungumza wakati akihitimisha hoja ya makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2021/22 ,Waziri Nchemba aliwahakikishia wabunge kuwa fedha hizo zilizoongezwa zinakwenda kutumika kwa melngo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wa Elimu ya Juu, Mwigulu amesema Serikali imeongeza kiasi cha sh. bilioni 70 ambazo zitasaidia kupeleka vyuo vya elimu ya juu wanafunzi takribani 11,000 walikoksa mkopo mwaka jana pamoja na wanafunzi 10,000 ambao walikadiriwa kukosa mkopo mwaka huu.

“Mwaka jana watoto 11,000 walikosa mikopo na walipokelewa na vyuo kwamba wana sifa za kuingia vyuoni, lakini walikosa masomo kwa sababu walikosa mikopo na wazazi wao hawana uwezo, wengine hawana wazazi na wakabaki majumbani na mwaka huu wanakadiriwa wangekosa mkopo zaidi ya
watoto 10,000.

"Na kwenye familia zetu mtoto amabye amefaulu mtihani huwa anakuwa faraja kwa familia na ukoo mzima ikitokea amekosa mkopo inaleta majonzi, kwa hiyo tunapendekeza kuogeza kwenye bilioni tulizopitisha kwenye wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia sh. bilioni 500,
tunaongeza takribani sh. bilioni 70 ambazo zinaenda sambamba kuwapeleka vyuoni watoto wote walikosa mikopo ambao wanafikia zaidi ya 21,000 ili nao wapate fursa hiyo na kuendelea ya elimu ya juu,"amesema.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu wake, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) wakiteta jambo kabla ya wabunge kuipitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2021/22, bungeni jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) akijibu hoja kabla ya kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2021/22 ya shilingi trilioni 36.66, bungeni jijini Dodoma.

Kuhusu Maboma ya Elimu, Waziri Nchemba amesema,kuanzia mwaka kesho shule za msingi zinaanza kutoa toleo la kwanza kwa wale wanafunzi walioandikishwa darasa la kwanza kwa mfumo wa elimu bila malipo, ambao wanaenda kumaliza darasa la saba na wanapaswa kuanza kidato cha kwanza

Kufuatia hali hiyo, amesema lazima miundombinu katika shule za sekondari iongezwe, kwani kutakuwa na mahitaji makubwa ya miundombinu katika shule hizo kutokana na uandikishaji kuongezeka katika shule za msingi.

“Tusipopanga kuwa na miundombinu kuanzia sasa ,takwimu zinaonesha tutakuwa na uhitaji wa vyumba vya madarasa kwa kiwango cha juu sana na hatutaweza kufanya kwa muda mfupi,”amesema Nchemba.

Kuhusu sekta ya afya, Waziri Nchemba amesema, sheria ya bima ya afya kwa wote inakuja na Wizara yake imependekeza ongezeko la sh. bilioni 50 kenye sekta hiyo, ambapo pamoja na mambo mengine fedha hiyo itafanya kazi ya kununua vifaa tiba na dawa.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) baada ya kuhitimisha kujibu hoja za wabunge kuhusu mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2021/22, jijini Dodoma.

Aidha, kuhusu sekta ya maji, amesema licha ya bajeti ya maji kupata fedha yake, lakini wameona kiongezwe kiasi cha sh. bilioni 207 ili kutatua tatizo la maji mijini na vijijini.

Pia amesema miradi mingine ya kimkakati kama SGR lazima ikamilike kwani ni miradi ya kimkakati na wabunge na watanzania waamini kwamba kazi hiyo itafanyika ipasavyo.

Kuhusu kodi hiyo, Waziri Nchemba amewatoa hofu wabunge na wananchi kwamba kazi hiyo inakwenda kufanywa na wataalam na kila mtu atalipa anachokistahili.

“Naomba nitoe rai kwa Watanzania, tusiiogope teknolojia imekuja kurahisisha kazi na wataalam wapo wametuhakikishia watafanya kazi hiyo vizuri na kodi itakusanywa kwa teknolojia ya kisasa na kila mtu atalipa anachokistahili,”amesema Nchemba.

Akitoa ufafanuzi wa eneo hilo, Mwigulu amesema, kumekuwa na kutokuelewana kwenye eneo hilo ambapo alisema mtumiaji wa chini atakatwa sh. 500 tu kwa mwezi na siyo kama ilivyoeleweka.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akipewa zawadi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), Bungeni jijini Dodoma baada ya kujibu hoja za wabunge kuhusu kodi zilizopendekezwa katika Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2021/22.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akiteta jambo na viongozi wa Wizara hiyo, wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Emmanuel Tutuba na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Adolf Ndunguru, baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Sh. trilioni 36.66, kwa mwaka 2021/22, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akipongezwa na Mama Salma Kikwete (Mb) baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Sh. trilioni 36.66, kwa mwaka 2021/22, bungeni jijini Dodoma.

“Makato ya kwenye simu upande wa muda wa maongezi kwa kiwango haikuwa imeeleweka kwa kile tulichokimaanisha, wapo waliodhania makato yanaenda kukatwa kwa kiwango siku kwenye mwezi husika, kwa maana kwamba itahesabiwa kuanzia tarehe ya kwanza ya mwezi mpaka tarehe ya mwisho na kwamba siku ukiweka salio inahesabiwa siku zote katika mwezi husika.


“Kwa maana hiyo ilikuwa inafananishwa na nipige tafu ambayo kama jana hukuweka ama jana ulitumia salio kwa kukopa basi ukiweka unakatwa kwanza ile ambayo siku ilishapita,la hasha sisi tulichopendekeza tumechukua takwimu za watumiaji wa simu tukaweka makundi yao,"amesema.

Amesema, kuna watumiaji wasiopungua milioni 8 ambao wana matumizi yao yasiyozidi sh. 1000 na wale wa sh. laki moja na kuendelea kwa hiyo tulichoweka kwa wale watumiaji wanaotumia viwango vya chini kwa mfano wa sh, 1000 kwenda chini atakatwa sh. tano pale anapoweka tu ,kwa wale wanaotumia sh. 7,500 hadi 10,000 atakatwa sh. 76 ,kwa wale wanaotumia sh. 10,000 hadi sh.25000 watakatwa sh. 112.

“Kama mtu anajiunga sh. 50,000 kwa mwezi anakatwa sh. 186 ni tofauti na ile hesabu tuliyokuwa tunapiga kama ni sh. 200 kwa siku maana yake kwa mwezi ni sh. 6,000 ilikuwa inatisha.

"Kwa kweli nachukia kuwapa mzigo Watanzania na kwa kweli nawahurumia Watanzania lakini nikasema nawahurumia zaidi wanaojifungulia vichakani, kwa mtu anayeweza kutumia 50,000 kwa mazungumzo akichangia sh.180 ili kuokoa maisha ya mama zetu kuna shida gani," amehoji Mheshimiwa Mwingulu.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Adolf Ndunguru (katikati) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Khatib Kazungu (kulia), wa pili kushoto ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Alphayo Kidata na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Mipango wa Wizara hiyo Bw. Moses Dulle, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu wake Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Taasisi za Wizara ya Fedha na Mipango, baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Sh. trilioni 36.66, kwa mwaka 2021/22, bungeni jijini Dodoma.

Ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa Watanzania wote kuwa lazima wajitoe kujenga nchi yao, kwani nchi itajengwa na watanzania wenyewe na hivyo ni lazima watanzania wenyewe wabebe majukumu hayo kama watanzania .

Pia amesema, Serikali imependekeza kuongeza shilingi 322 kwenye barabara kwenye maeneo ambayo hayapitiki .

“Tulishapitisha bajeti ya TARURA zaidi ya sh. bilioni 400,zile zitafanya kazi zake za kawaida lakini tunapendekeza tuongeze ziada ya zile sh. bilioni 400 na bahati nzuri zile zinakwenda moja kwa moja kwenye mfuko ili tukafungue maeneo ambayo hayapitiki mijini na vijijini bado tuna maeneo mpaka karne hii lakini hakuna gari linaweza likafika pale,sasa hii hali tunataka tuiondoe,”amesema.

Amesema, kutokana na ongezeko hilo kila jimbo nchini litapata zaidi ya sh.bilioni moja kwa ajili ya matengenezo ya barabara za TARURA zitapitika wakati wote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here