Mtangazaji maarufu Fredwaa wa Clouds FM afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mtangazaji maarufu nchini Tanzania, Fred Fidelis maarufu kama Fredwaa amefariki leo mkoani Dar es Salaam.
Taarifa za awali zimeudokeza mtandao huu wa Diramakini Blog kuwa, Fredwaa amefariki baada ya kupata ajali ya gari leo huko Kawe Manispaa ya Kinondoni.

Wakati wa uhai wake, Fredwaa amewahi kufanya kazi Radio Free Africa ya jijini Mwanza,Times Fm pamoja na CloudsFM ya mkoani Dar es Salaam.

Fredwaa baada ya kuhamia Clouds Fm alikuwa akisikika sana katika kipindi cha Power Breakfast, akiungana na Mbwiga, Gerald Hando, Bonge na wengine. 

Mtangazaji huyo alijizolea umaarufu katika kipindi chake cha asubuhi pale RFA, ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa na segment inaitwa Vodacom Top Five.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema chanzo cha ajali hiyo ni ulevi na  wanamshikilia dereva wa gari hilo.

“Inaonekana dereva alikuwa amelewa wakati akiendesha gari liliacha njia na kuingia mtaroni eneo la Tanganyika Packers karibu na sehemu ambayo Mchungaji Boniphace Mwamposa huwa anatoa neno, mtangazaji (Fredwaa) alifariki ila dereva tunamshikilia,” amesema Kamanda.

Post a Comment

0 Comments