Mzee Matata wa Mizengwe ITV afariki

Mwigizaji wa Kikundi cha Maigizo cha Kashkashi kinachorusha mchezo wao wa kuchekesha wa Mizengwe kupitia Televisheni ya ITV, Jumanne Alela maarufu Mzee Matata amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 16, 2021 Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Ilala mkoani Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu toka Juni 13, mwaka huu.
Taarifa ya kifo chake zimethibitishwa leo Jumatano Juni 16, 2021 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha.

Aligaesha amesema, msanii huyo amefariki dunia jana saa tano na nusu baada ya kulazwa katika hospitali hiyo tangu Juni 13, 2021.

Kwa mujibu wa mwigizaji maarufu nchini, Madebe, mazishi ya Mzee Matata yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Buguruni Malapa jijini Ilala, Dar es Salaam.

“Mwanatasnia mwenzetu Mzee Jumanne Alela (Mzee Matata) maziko yake yatafanyika kesho saa saba mchana kwenye Makaburi ya Buguruni Malapa.Msiba upo kwa ndugu zake, Chamazi kwa Mkongo,”ameeleza Madebe.

Post a Comment

0 Comments