NA MWANDISHI DIRAMAKINI
KIKAO cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimefanyika leo kikiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Jijini Dodoma ambacho kilihudhuriwa na viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichokutana leo Juni 22,2021 katika Ukumbi wa Jakaya Convention Centre Jijini Dodoma.Kikao hicho ambacho ni
cha kawaida na cha kwanza kwa Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Samia Suluhu
Hassan pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo kimefanyika
kujadili masuala mbali mbali ya chama hicho cha CCM.
Kikao hicho
kimefanyika baada ya Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa, kilichofanyika jana Juni 21,2021 chini ya Mwenyekiti wake Katibu
Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo huko katika ukumbi wa NEC, White House
Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo Juni 22,2021, alipokua akielekea Nchini Msumbiji kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya SADC unaotarajiwa kuanza kesho.
Tags
Habari