REA YABAINISHA MIKAKATI KUONGEZA UPATIKANAJI NISHATI VIJIJINI

Na Veronica Simba, REA

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umebainisha mikakati yake kadhaa inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma za nishati vijijini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka akizungumza wakati wa semina iliyoratibiwa na Wizara ya Nishati ili kuwajengea uelewa kuhusu sekta ndogo ya umeme Wajumbe wa Kamati hiyo Juni 10, 2021 jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati Wakili Stephen Byabato na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Japhet Hasunga.

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga ameeleza mikakati hiyo leo, Juni 10, 2021 jijini Dodoma, wakati akiwasilisha Mada kuhusu Majukumu ya Wakala huo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), katika Semina ya kuwajengea uelewa kuhusu sekta ndogo ya umeme, iliyoratibiwa na Wizara ya Nishati.

Ameitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuhamasisha na kuwezesha ushiriki wa sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya nishati maeneo ya vijijini pamoja na kushirikisha Taasisi za Fedha katika uwekezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Vilevile, Mhandisi Maganga ameeleza mkakati mwingine kuwa ni kuendelea kuhamasisha utekelezwaji wa miradi ya nishati jadidifu kutoka vyanzo vya asili vinavyopatikana maeneo ya vijijini na hasa kwenye visiwa.
Naibu Waziri wa Nishati Wakili Stephen Byabato akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu sekta ndogo ya umeme, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyofanyika Juni 10, 2021 katika Ukumbi wa Ofisi ndogo za Wizara zilizopo Kikuyu, Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu sekta ya ndogo ya umeme, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyofanyika Juni 10, 2021 katika Ukumbi wa Ofisi ndogo za Wizara zilizopo Kikuyu, Dodoma.

Aidha, amesema kuwa upo mkakati wa kushirikiana na Asasi za Kiraia na zisizo za Kiserikali katika utekelezaji wa miradi ya nishati bora maeneo ya vijijini.

Akieleza zaidi, amesema mkakati mwingine ni kuendeleza upanuzi wa mifumo ya umeme ya gridi ya Taifa kufikia maeneo mengi zaidi ya vijijini kwa kuwatumia wakandarasi binafsi wenye uwezo wa kutekeleza miradi kwa kiwango kinachotakiwa.

Ameongeza kuwa REA inatekeleza mkakati wa kuibua na kupanga maeneo yatakayopelekewa miradi kutokana na vipaumbele vya taasisi pamoja na Taifa kwa kuzingatia mikoa ambayo imefikiwa na huduma ya umeme kwa viwango vidogo.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali kupitia Wakala huo, kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Juni 10, 2021 katika Ukumbi wa Ofisi ndogo za Wizara zilizopo Kikuyu, Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Busega, Simon Songe akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu sekta ndogo ya umeme, Wajumbe wa Kamati hiyo Juni 10, 2021 katika Ukumbi wa Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo Kikuyu, Dodoma.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Maganga ameileza Kamati ya PAC kuhusu hali ya upatikanaji wa huduma za umeme vijijini ambapo amebainisha kuwa Wakala umekuwa ukitekeleza miradi ya nishati vijijini ili kuboresha maisha ya wananchi waishio maeneo hayo.

Akifafanua, ameeleza kuwa Vijiji 8,538 kati ya 12,268 vya Tanzania Bara sawa na asilimia 69.6 vimefikiwa na miundombinu ya umeme na kuongeza kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei 2021, jumla ya vijiji 10,328 kati ya 12,268 vimefikiwa na miundombinu ya umeme.

“Wakala umejiwekea malengo ya kufikisha miundombinu ya umeme kwenye vijiji vyote Tanzania Bara ifikapo Desemba 2022 na kuhakikisha hali ya upatikanaji wa huduma za umeme inafikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2030,” amesema.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Katavi, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu sekta ya ndogo ya umeme Wajumbe wa Kamati hiyo Juni 10, 2021 katika Ukumbi wa Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo Kikuyu, Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nkasi, Aida Khenan akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu sekta ndogo ya umeme, Wajumbe wa Kamati hiyo Juni 10, 2021 katika Ukumbi wa Ofisi ndogo za Wizara ya Nishati zilizopo Kikuyu, Dodoma.
Msaidizi Binafsi wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Deogratius Nagu (kushoto) na Msaidizi Binafsi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Pius Gaspar, wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu sekta ndogo ya umeme, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyofanyika Juni 10, 2021 katika Ukumbi wa Ofisi ndogo za Wizara zilizopo Kikuyu, Dodoma.
Meneja Tathmini na Usimamizi wa Miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Romanus Lwena akifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu sekta ndogo ya umeme, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyofanyika Juni 10, 2021 katika Ukumbi wa Ofisi ndogo za Wizara zilizopo Kikuyu, Dodoma.
Viongozi na Wataalam mbalimbali wa Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa semina ya kuwajengea uelewa kuhusu sekta ndogo ya umeme, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyofanyika Juni 10, 2021 katika Ukumbi wa Ofisi ndogo za Wizara zilizopo Kikuyu, Dodoma.

Awali, akizungumza katika Semina hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Naghenjwa Kaboyoka aliipongeza REA, TANESCO na Wizara ya Nishati kwa ujumla, kwa kazi nzuri inayoendelea kufanyika kuunganisha umeme katika maeneo mbalimbali nchini hususan kwa wananchi walioko vijijini.

Naye Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, aliwahakikishia Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa, Wizara yake itaendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha watanzania wote wanafikiwa na huduma hiyo muhimu ya umeme.

Aliwaomba Wawakilishi hao wa wananchi kuwa Mabalozi wazuri wa masuala ya nishati katika majimbo yao kwa kuwahamasisha wakazi wa maeneo hayo wanayoyawakilisha kuchangamkia fursa za kuunganisha umeme katika kaya na maeneo yao ya biashara ili kuboresha maisha yao.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali amewashukuru Wabunge hao kwa mwitikio wao katika kushiriki Semina hiyo na kuahidi kuwa Wizara itazingatia michango na maelekezo mbalimbali waliyoyatoa ili kuendelea kuboresha sekta ndogo ya umeme na nishati kwa ujumla.

Semina hiyo imefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara zilizopo Kikuyu jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments