Simba SC yawachezesha kwata maafande wa Polisi Tanzania yaibuka 1-0

NA GODFREY NNKO 

Baada ya dakika moja ya kumkumbuku ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zambia,Dkt. Kenneth Kaunda ambaye alifariki siku ya Alhamisi ya Juni 17, 2021huko jijini Lusaka Zambia, katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza, Wekundu wa Msimbazi wamewachezecha kwata maafande wa Polisi Tanzania.
Simba SC walionekana kutawala mechi hiyo na kufanikiwa kupata bao lililofungwa na Luis Miquisone dakika 27 kwa mpira wa faulo.

Licha ya juhudi za maafande wa Polisi Tanzania katika mtanange huo, mambo hayakuwawia vema kama walivyodhamiria.

Matokeo hayo yameendelea kuwafanya Wekundu wa Msimbazi kuwa wababe kwa maafande hao, kwani michezo yote minne ukiwemo na wa leo wametembeza vipigo tangu walipopanda daraja misimu miwili kwa sasa.

Mtanange huo katika kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikifanya mabadiliko.

Wekundu wa Msimbazi waliwatoa Mugalu, Bwalya na Yassin na kuingia Kagere, Nyoni na Hassan Dilunga huku maafande wakimtoa Daluwesh Saliboko na nafasi yake kuchukuliwa na Jimmy Shoji.

Licha ya mabadiliko hayo kutokuwa na faida kwa pande zote baada ya dakika 90 za Mwamuzi, Ahamad Simba kutoka Kagera kumalizika, maafande walipata nafasi moja ambayo haikuzaa matunda.

Alama tatu za leo, zinawafanya Simba SC kung'ang'ania kileleni kwa alama 70 nafasi ya tatu ikiwa chini ya Azam FC ambayo imefikisha alama 63 baada ya kucheza mechi 31, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa alama moja na Yanga SC ambao pia wana mechi moja mkononi.

Post a Comment

0 Comments