Magazeti leo Desemba 6,2025

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho (Mb) tarehe 05 Desemba 2025, amefanya ziara ya Kikazi kutembelea Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Msalato Dodoma kwa ajili ya kuzungumza na kujitambulisha kwa Maafisa, Askari pamoja na Watumishi wa Umma wa Makao Makuu ya Jeshi.
Mara baada ya Kuwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi, Mhe Dkt. Rhimo alipokelewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda aliyeongoza Maafisa na Askari pamoja na watumishi wa umma kumlaki Waziri wa Ulinzi na JKT, na baadaye kuzungumza na Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma waliohudhuria hafla hiyo ya kumlaki Waziri wa Ulinzi na JKT Makao Makuu ya JWTZ.

Katika hotuba yake, Waziri Nyansaho amemuhakikishia Mkuu wa Majeshi utayari wa Serikali ya Awamu ya Sita,inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania linaendelea kuwezeshwa ili liendelee kutimiza Majukumu yake ya Ulinzi wa Taifa. 

Waziri Rhimo akawaambia Maafisa na Askari wa JWTZ kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa JWTZ na taasisi zake kufikia malengo yanayokusudiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here