UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA BAGAMOYO HADI KIGAMBONI

TAARIFA KWA UMMA

16.06.2021

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na wananchi wa Bagamoyo hadi Kigamboni kuwa kutakua na ukosefu wa huduma ya maji kuanzia tarehe 17/6/2021 hadi 18/6/2021.

Sababu: Marekebisho madogo katika mfumo wa mtambo wa maji wa Ruvu Chini.

Maeneo yatakayoathirika;

Mji wa Bagamoyo, Vijiji vya Zinga, Kerege, Mapinga, Bunju, Boko, Mivumoni, Kawe, Tegeta, Salasala, Jangwani, Kunduchi, Mbezi Beach, Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Kijitonyama, Oysterbay, Magomen, Upanga, Kariakoo, Katikati ya jiji, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Muhimbili, Kigamboni Navy na Ferry

Tafadhali hifadhi maji ya kutumia katika kipindi hicho ili kupunguza usumbufu. DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Kwa taarifa zaidi, wasiliana nasi, kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064(bure) au0735 202121(WhatsApp tu)


Imetolewa na

Kitengo cha Mawasiliano na Jamii

Post a Comment

0 Comments