Diwani Rehema Mandingo atekeleza jambo Mikocheni

Na Anneth Kagenda, Diramakini Blog

VIONGOZI nchini wameshauriwa kuendelea kutimiza ahadi zao wanazowaahidi wananchi kwa madai kuwa kufanya hivyo kutakuwa ni kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Ushauri huo ulitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Mtaa wa Darajani Kata ya Mikocheni ambaye hivi sasa ni Diwani Viti Maalum katika Wilaya ya Kinondoni, Rehema Mandingo wakati akizungumza na Diramakini Blog.

Mwenyekiti huyo amesema, katika kumuunga mkono Rais Samia pamoja na kamati mzima ya Ulinzi na Usalama ilifanikiwa kujenga choo ili askari wai waweze kufanya kazi katika mazingira mazuri na kutoa huduma bora na kwa ufasaha zaidi.

"Lakini pia awali kulikuwa na changamoto ya askari kutokuwa na mazingira yasiyo rafiki, hivyo nilifanikiwa kuboresha Kituo cha Polisi lengo likiwa ni kuwafanya askari wetu wafanye kazi zao katika mazingira mazuri," amesema Diwani Mandingo.

Aidha, amesema kuwa mbali na hilo pia aliona upo umuhimu wa kuwaboreshea wananchi maeneo ya kupunzika wakati wakisubiri kutatuliwa matatizo yao hivyo akanunua viti vya kukaa.

"Pia tulikuwa na changamoto kubwa ya mitaro ya kutiririsha maji ya mvua kwa hivyo kwa kushirikiana na Serikali nayo nilifanikiwa kuijenga jambo lililosaidia kuwapunguzia adha ya mafuriko kwenye mitaa ya wananchi wetu,"amesema.

Aidha, ameema kuwa awali kauli mbiu yake ilikuwa ni 'niliahidi nimetekeleza' na kwamba hiyo yote ni kuhakikisha anafanya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa nafasi aliyoaminiwa ya Uenyekiti wa Serikali ya Mtaa kwa kipindi cha 2019-2021.

Hata hivyo, amesema kwa wakati huu ambao yeye ni Diwani Viti Maalum kutoka Wilaya ya Kinondoni ataendelea kuwatumikia watu wa Mikocheni na Wilaya ya Kinondoni.

"Wakati nikitekeleza majukumu yangu ya kuwaletea wananchi maendeleo naomba wananchi wanipe ushirikiano wa hali na mali ili tuweze kusonga mbele zaidi na kwa mafanikio makubwa kama anavyotaka Rais wetu," amesema Diwani huyo.

Post a Comment

0 Comments