🔴LIVE:Soko la Kariakoo DAR ES SALAAM linateketea kwa moto

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Soko Kuu la Kariakoo lililopo jijini Ilala mkoani Dar es Salaam linaungua moto usiku huu huku jitihada za kuuzima zikiendelea kutoka kwa wadau mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ni miongoni mwa viongozi waandamizi wa Serikali wanaosaidia katika uokoaji huu.

Mheshimiwa Makalla amesema moto huo umeanza kuwaka saa 3:30 ya leo Julai 10,2021 na chanzo bado hakijajulikana hadi sasa.

 

Post a Comment

0 Comments