NECTA yatangaza wanafunzi 10 bora Kidato cha Sita 2021

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2021 na kutaja wanafunzi kumi bora waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde amemtaja Perucy Astus Mussiba kutoka shule ya Canossa, Dar es Salaam kuwa kinara wa matokeo hayo, katika masomo ya sayansi mchepuo wa PCB.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Donard Rulers Mosile kutoka Shule ya Sekondari Kisimiri (Arusha) kutoka PCB. Cretus Amos Mihayo kutoka Tabora Boys (Tabora) PCB akishika nafasi ya tatu akifuatiwa na Ismail Mtumwa kutoka Kibaha Sekondari(Pwani) PCM aliyeshika nafasi ya nne.

Nafasi ya tano imechukuliwa na Olais Julius Mollel kutoka Kisimiri (Arusha) PCM akifuatiwa na Geofrey Sanga aliyeshika nafasi ya sita kutoka Tabora Boys (Tabora) PCM.

Anord Msanga kutoka Tabora Boys (Tabora) PCM akichukua nafasi ya saba Caroline Mpale amechukua nafasi ya nane kutoka Canossa Sekondari (Dar es Salaam) akichukua mchepuo wa PCM.

Nafasi ya tisa na kumi imechuukuliwa na wanafunzi kutoka Feza Boys (Dar es Salaam) PCM John Bugeraha aliyechukua nafasi ya tisa na Harry Mshana aliyechukuwa nafasi ya kumi.

Matokeo hayo yametangazwa leo Jumamosi Julai 10, 2021 jijini Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments