Makamu wa Rais aagiza kusimamishwa kazi Mkurugenzi wa Nanyumbu, Hamis Hassan Dambaya


NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, leo Julai 24, 2021 amefanya ziara ya kushtukiza katika stendi ya Mabasi ya Mangaka iliyopo Wilaya ya Nanyumbu.
Mkurungenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, Hamis Hassan Dambaya

Makamu wa Rais amekasirishwa na uongozi wa Wilaya kufanya upotevu mkubwa wa fedha usiolingana na matokeo ya ujenzi wa mradi huo.

Ujenzi wa majengo ya stendi hiyo umetumia shilingi bilioni 2.2 kiasi ambacho Makamu wa Rais amesema hakilingani na ujenzi huo.

Makamu wa Rais amemuagiza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Festo Dugange kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, Hamis Hassan Dambaya ili kupisha uchunguzi kutoka vyombo husika.

Amesema, viongozi hawana budi kusimamia fedha za serikali zinazopelekwa katika maeneo yao ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Post a Comment

0 Comments