Mbunge Askofu Gwajima, wenzake wakalia kuti kavu CCM

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Chama Cha Mapinduzi kinafuatilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha Umma na kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Samia Suluhu na maadili ya chama.


CCM inawahakikishia wanachama na watanzania kuwa, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote ambao wanatumia nafasi hiyo kusukuma ajenda zao binafsi, kwa mujibu wa Katiba, kanuni za maadili na uongozi za CCM.

Kauli hii ya CCM imetokana na kauli kinzani zinazotolewa na baadhi ya makada wake katika masuala ambayo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekwishayatolea maelekezo ikiwemo suala la tozo na COVID-19.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi.

Post a Comment

0 Comments