Waziri Mkuu aagiza kasi iongezeke ujenzi wa Barabara ya Ruangwa-Nanganga

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation ya China inayojenga barabara ya kutoka Ruangwa hadi Nanganga na kuwataka waongeze kasi ili waweze kukamilisha kwa wakati.

Ametoa agizo hilo leo Jumatatu, Julai 26, 2021 alipokutana na viongozi hao katika kijiji cha Namahema wilayani Ruangwa. Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 53.2 inatarajiwa kugharimu kiasi cha sh bilioni 59.28 na imepangwa kukamilika Novemba 2022.
Waziri Mkuu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa akizungumza na Meneja Mkazi wa Kampuni ya China Railway 15 Group Corporation, Su Jinlan (kushoto) ambayo inajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Nanganga – Ruangwa, katika Kijiji cha Namahema Ruangwa, Julai 26, 2021. Wa tatu kushoto ni Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi, Mhandisi Ephata Mlavi na wa pili kulia ni Mhandi wa Barabara Kuu, Wambura Isareba. Katika mazungumzo hayo Mheshimiwa Majaliwa alipokea taarifa kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.


Mheshimiwa Majaliwa amesema barabara ya Ruangwa – Nanganga ni muhimu kwani kukamilika kwake kutarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo yakiwemo mazao mbalimbali ya kilimo hivyo kuchangia katika kukuza uchumi na kuongeza tija kwa wakulima.

Kwa upande wake, Meneja Mkaazi wa kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation Bi Su Jinlan amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba wataongeza kasi ya ujenzi wa mradi wa barabara hiyo na kwamba itakamilika kwa wakati. Hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 18 ya utekelezaji.

Meneja huyo amesema kuwa kampuni yao imejipanga ipasavyo na wanatarajia kuongeza vifaa vya kufanyia kazi ili waweze kukamilisha ujenzi mradi kama ilivyokusudiwa. Pia amewashukuru wananchi wa wilaya hiyo kwa ushirikiano wanaoutoa kwao.
Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa mpira wa miguu wilaya ya Ruangwa kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo, Julai 26, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amezungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Gogovivu wilayani Ruangwa ambapo ametumia fursa hiyo kuwasisitiza waendelee kuiunga mkono Serikali katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Akizungumzia sekta ya elimu, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea na mchakato wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kutolea elimu ukiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa. “Leo hii kata zote za wilaya ya Ruangwa zina shule za sekondari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news