OFSI YA CAG YATIMIZA MIAKA 60

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

OFSI ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imesherehekea miaka 60 tangu kuanzishwa kwake huku ikieleza mafanikio makubwa yakiwemo ya ushirikiano mkubwa kutoka kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali na Muongozo wa Kuwajengea Uwezo Wabunge wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu ofisi hiyo ianzishwe nchini. Kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kicheere.

Akizungumza katika hafla hiyo jijini Dodoma Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kicheere amesema kuwa, majukumu ya ofsi hiyo yameendelea katika uwajibikaji na uwazi hasa kwenye rasilimali fedha.

Amesema kuwa, kumekuwa na ushirikiano baina ya ofsi na taasisi mbalimbali za binafsi na Serikali pamoja na Bunge ambalo limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha linatekeleza jukumu lake la kujadili na kufanyia kazi ripoti za CAG kwa wakati.

Amesema, ofsi ya CAG itaendelea kuwa jicho kali na angavu litakalotazama mapato na matumizi ya Serikali ili kulisaidia Bunge kusimamia na kuishauri Serikali Kkatika usimamizi wa rasilimali za umma.

Aidha,amesema ofisi hiyo kipindi cha miaka mitano imeweka mikakati ya kuboresha utendaji kazi bora ikiwa ni pamoja na kuzidi kuongeza imani kwa umma, kujenga uelewa wa pamoja na mafunzo mbalimbali kwa Bunge ili kuzidi kudumisha mahusiano na misingi imara.

Awali akiongea katika hafla hiyo, mgeni rasmi Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai amesema ofisi ya CAG imekuwa msaada mkubwa katika kuibua mambo mbalimbali ya miradi na wabadhirifu wa fedha huku akiitaka ofisi hiyo kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yake kwani ndiye tegemeo na nyenzo muhimu.

Aidha, ameongeza kama Bunge taarifa inayotoka huko ni nyenzo muhimu katika kutimiza majukumu yao ya kuisimamia Serikali hususani kutokana na taarifa upata nafasi za kujadili, kuishauri na kutambua miendendo ya miradi inayoendelezwa na serikali na kufuatilia kwa kina.

"Tunashukuru sana Bunge letu lina ushirikiano mzuri na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu niwaombe mnapotimiza miaka 60 tambua kuwa mmepewa dhamana kubwa na Serikali mfanye kazi kwa maslahi ya nchi yetu.

"Muendelee kufanya kazi kwa ubunifu zaidi, weledi,uadilifu na sisi Bunge tutaendeleza kudumisha umoja na mshikamano ili tulisongeshe Taifa letu mbele,"amesema Spika Ndugai.

Ikumbukwe kuwa Ofsi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilianzishwa mwaka tangu mwaka 1961.

Post a Comment

0 Comments