Serikali yatoa maelekezo kuhusiana na homa ya ini

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

KATIKA kuadhimisha Kilele cha Siku ya Homa ya Ini Duniani, Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imeitaka jamii na taasisi mbalimbali kuwa na kasumba ya kupima, kupata chanjo ya ugonjwa huo ambao kwa Tanzania maambukizi yapo kwa asilimia nne.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Homa ya Ini kutoka Wizara ya Afya Dkt. Baraka Nzobo wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma.

Daktari Nzobo amesema kuwa, jamii nyingi hapa nchini haina utamaduni wa kupima au kupata chanjo ya homa ya ini kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya ugonjwa huo.

"Mtu yuko tayari kupima ugonjwa wa UKIMWI au kutumia kinga akijikinga na UKIMWI ama mimba ila asijue kama anajikinga na ugonjwa wa homa ya ini pia, kwani ugonjwa wa ini unaweza kuupata unapofanya mapenzi bila kinga au kunyonyana ndipi,"amesema Dkt.Nzobo.

Pia amesema wajawazito wana uwezo wa kuwaambukizwa pale anapokuwa nao, hivyo wajawazito wanapaswa kwenda kwenye vituo vya afya kupima mara kwa mara kujua afya zao na kupata kizazi ambacho hakina maambukizi.

Akielezea dalili za maambukizi ya homa ya ini ameema ni ngozi ya mtu kuwa ya njano au kwenye macho,kupata mkojo ambao ni mweusi ,uchovu uliokithiri,kichefuchefu na kutapika na maumivu makali ya tumbo na kupunguza uzito.

Makundi ambayo yako hatarishi ni madaktari,wahudumu wa mochwari,manesi na wauguzi wa kuzalisha akina mama, wanafunzi vyuoni wanaokwenda kufanya kivitendo,hospitalini,vituo vya wazee,walemavu,saluni,wafanyakazi kwenye taasisi, madereva wa masafa marefu .

Njia za kujikinga ni kupata chanjo ili kuepukana na maambukizi hayo ambapo kila mzazi pale mtoto anapozaliwa kuhakikisha anapata chanjo zote ambapo kwa hapa Tanzania chanzo hiyo ilianza kutolewa mwaka 2002.

Hata hivyo, Dkt. Nzobo ametoa wito kwa taasisi zote kupata chanjo huku akizitaka ziepuke kushirikishana vitu vya ncha kali na kuepukana na kufanya mapenzi bila kutumia kinga pamoja na kutumia vyoo safi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news