YALIYOJIRI TUME YA UTUMISHI WA UMMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO JULAI 23, 2021


Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji (mstaafu) Mheshimiwa Dkt. Steven J. Bwana (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi Hodari wa Tume baada ya kuwakabidhi Hati zao za Mfanyakazi Hodari wa Tume ya Utumishi wa Umma kutoka TUGHE kwa mwaka 2020/2021. Kushoto ni Bw. Nyakimura Muhoji, Katibu wa Tume. Hafla ya kuwakabidhi Hati hizo imefanyika leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na PSC).
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji (Mstaafu) Mheshimiwa Dkt. Steven J. Bwana (kushoto) akizungumza na Wafanyakazi Hodari wa Tume ya Utumishi wa Umma (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam baada ya kuwakabidhi Hati zao za Ufanyakazi Hodari kwa mwaka 2020/2021 zilizotolewa na TUGHE, pamoja nae ni Bw. Nyakimura Muhoji (wa pili kushoto) Katibu wa Tume, Bw. Gift Lyimo (Afisa Utumishi) na Bw. Charles Mulamula, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume. (Picha na PSC).
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana (kushoto) akimpongeza baada ya kumkabidhi Hati ya Mfanyakazi Hodari iliyotolewa na TUGHE, Bi. Nuru Abdallah Hanti (kulia) Afisa Utumishi (Idara ya Rufaa na Malalamiko) Tume ya Utumishi wa Umma aliyechaguliwa kuwa mfanyakazi bora na hodari wa Tume kwa mwaka 2020/2021, hafla imefanyika leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na PSC).
Dkt. Garvin Kweka (wa kwanza kushoto) kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kitengo cha Figo akifafanua jambo kwa Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Umma leo wakati wa mafunzo kuhusu UKIMWI/VVU mahali pa kazi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. (Picha PSC).
Bibi Celina Maongezi (kulia) Katibu Msaidizi, Tume ya Utumishi wa Umma akipima afya na VVU kwa hiari wakati wa mafunzo kuhusu UKIMWI yaliyotolewa leo kwa Watumishi wa Tume, kushoto ni Dkt. Hamdani Kanaya kutoka Maabara ya TAMISEMI. (Picha na PSC).
Dkt. Garvin Kweka kutoka Kitengo cha Figo, Hospitali ya Taifa Muhimbili akifafanua jambo kwa Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Umma (hawapo pichani) wakati wa mafunzo kuhusu UKIMWI/VVU kwa Wafanyakazi wa Tume leo Jijini Dar es Salaam.
Bw. Nyakimura Muhoji, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma akiwashukuru baadhi ya Wanachama wa TUGHE Tawi la Tume ya Utumishi wa Umma (hawapo pichani) waliofika Ofisini kwake leo kutoa shukrani kwa kuwa mwanachama wa TUGHE na kwa kutambua mchango wake alioutoa kwa Tume.

Post a Comment

0 Comments