KMC FC YASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI NA MASITA SPORTS WEAR

Timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC FC imesaini mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Kusambaza vifaa vya michezo Duniani MASITA SPORTS WEAR ya Nchini Uholanzi kwa ajili ya kusambaza vifaa vya timu kwa miaka miwili.
Mwenyekiti wa Timu ya KMC FC , Kheri Misinga wapili kulia , Mkurugenzi Mtendaji wa Level Up, ndugu. Daudi Aboud watatu katikati wakiwa wameshika mkataba wa Makubaliano ya usambazaji wa vifaa vya michezo ya KMC FC uliosaniwa leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Level Up Daud Aboud akisaini mkataba wa makubaliano ya usambazaji wa vifaa vya michezo ya KMC FC kwa kipindi cha miaka miwili.
Katibu wa KMC FC Walter Harison akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Level Up ,Ndugu. Daud Aboud wakiwa wameshika Mkataba wa Makubaliano ya usambazaji wa vifaa vya michezo ya Timu ya KMC FC.

Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dar Es Salaam leo chini ya Kampuni ya Level Up ambao ndio wawakilishi wenye hati miliki ya kusambaza vifaa vya MASITA kwa ukanda wa Africa Mashariki na Kati.

Katibu Mkuu wa KMC FC Mr Walter Harson amesema MASITA ni kampuni bora na wanategemea ubora zaidi utaongezeka baada ya kufanya kazi kwa msimu uliopita kwa kiwango kikubwa.

Awali wakisaini mkataba huo , Mkurugenzi Mtendaji wa Level Up Mr Daud Aboud amesema ni nafasi kubwa kwao kufanya kazi na timu kubwa kama KMC FC na wana imani watashirikiana vizuri katika makubaliano hayo na hivyo kutimiza malengo ya kuhakikisha wanaleta vifaa bora vinavyotengenezwa na kampuni hiyo ya MASITA.

Imetolewa leo Agosti 11


Na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mahusiano wa KMC FC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news