Mbunge Tabasamu:Hospitali ya Sengerema imezidiwa na wagonjwa wa UVIKO-19

Na Robert Kalokola, Dirmakini Blog

Mbunge wa Jimbo la Sengerema, Hamis Tabasamu ameomba Serikali kuingilia kati kunusuru uhaba wa mitungi ya Hewa ya Oksijeni ambao unaikumba Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema baada ya wagonjwa wa Uviko-19 kuongezeka baada ya wimbi la tatu linalosumbua Dunia kwa sasa.
Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu akimkabidhi Marry Jesee hundi ya shilingi milioni 3.5 kwa ajili gharama za kujaza mitungi ya hewa ya Oksijeni 100. (Picha Robert Kalokola/Diramakini Blog).

Amesema kwa sasa hospitali hiyo inapokea wagonjwa kutoka wilaya zaidi tano kutoka Mkoa wa Mwanza na Mkoa wa Geita hivyo kuiomba Wizara ya Afya,Jinsia,Wazee na Watoto kupeleka huduma maalum ya ziada kama zile zinazotolewa kwenye hospitali za rufaa ili kunusuru wagonjwa waliopo kwa sasa.

Hamis Tabasamu amesema hayo wakati akitoa msaada wa shilingi milioni 3.5 kwa ajili kwa hospitali hiyo kwa ajili ya gharama za kujaza mitungi ya Oksijeni mia moja (100) ambayo ni kwa ajili ya wagonjwa wanaosumbuliwa na Uviko-19.

Aidha, amesema kuwa gharama za kuendesha mitungi hiyo ya Oksijeni katika hospitali hiyo ni kubwa kulinganisha na idadi ya wagonjwa wanaolazwa kwa mwezi kwani kila mtungi mmoja unatumia zaidi ya elfu 35 kujazawa.
Mbunge wa Sengerema (mwenye kofia) akikabidhi sabuni katoni mbili kwa ajili ya kunawa mikono, Klorini kwa ajili ya kupulizia na barakoa 1000 kwa ajili ya watumishi wa Hospitali Teule Sengerema. (Picha: Robert Kalokola/Diramakini Blog).

Marry Josee Mganga Mkuu Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema amesema kuwa, hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu wa mitungi ya Hewa ya Oksijeni baada ya wagonjwa wanaohitaji msaada wa upumuaji kwa kutumia mitungi hiyo kuwa kubwa katika kipindi cha miezi miwili katika kipindi hiki.

Ameongeza kuwa, hospitali hiyo kwa sasa ina jumla ya mitungi ya Oksijeni 19 wanaohitaji Mitungi ya oksijeni kwa sasa mitungi inayohitajika ni 60 kwa mwezi,hali inayowafanya kushindwa kutoa huduma kwa baadhi ya wangonjwa wenye uhitaji huo ambapo mgonjwa mmoja kwa siku anahitaji mitungi.

Mbali na kutoa msaada wa milioni 3.5 kwa ajili ya kujaza Mitungi ya Oksijeni,pia ametoa sabuni ya unga katoni mbili kwa ajili ya kunawa mikono kwa watu wanaofika Hospitali,Klorini kwa ajili ya kupulizia maeneo mbalimbali ya majengo ya hospitali hiyo pamoja na barakoa 1,000 kwa watumishi wa hospitali hiyo.
Katibu wa afya Wilaya ya Sengerema idara ya Afya Jimbo Katoliki la Geita Leonard Masawe amesema kuna serikali ione umuhimu wa kupandishwa hadhi Hospitali hiyo kuwa ya Rufaa kwani maandalizi yalishaana kufanyika.

Amesema, baadhi ya maandalizi kama idadi ya vitanda na huduma nyingine za kibingwa ziko sawa na baadhi ya hospitali nyingine ambazo zina hadhi ya rufaa na zinapata huduma zaidi kuliko hospitali teule kama ilivyo kwa Hospitali ya Sengerema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news