Naibu Waziri Dkt.Mabula ashiriki maziko ya hayati Elias Kwandikwa

Na Munir Shemweta, KAHAMA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula ameungana na viongozi wengine wa serikali katika maziko ya aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hayati Elias Kwandikwa.

Maziko hayo yamefanyika leo tarehe 9 Agosti 2021 katika kijiji cha Butibu kilichopo katika halmashauri ya Ushetu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hayati Elias Kwandikwa yaliyofanyika kijiji cha Butibu, Ushetu mkoani Shinyanga leo tarehe 9 Agosti 2021. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na viongozi wengine wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hayati Elias Kwandikwa yaliyofanyika kijiji cha Butibu, Ushetu mkoani Shinyanga leo tarehe 9 Agosti 2021. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hayati Elias Kwandikwa katika mazishi yaliyofanyika kijiji cha Butibu, Ushetu mkoani Shinyanga leo tarehe 9 Agosti 2021. ( PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI)

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria maziko hayo ni Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro, Mawaziri, Wabunge na viongozi wa vyama vya Siasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news