Mtangazaji maarufu Juma Ahmed Baragaza wa RFA na Star TV afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mtangazaji maarufu wa Radio Free Afrika na Star Tv ya jijini Mwanza,Juma Ahmed Baragaza amefariki dunia leo Agosti 7,2021.
"Baragaza ameondoka na hakika ameacha 'gap' kubwa sana katika hii tasnia,kwani alikuwa mbunifu katika vipindi na utangazaji wake,"mmoja wa ndugu wa karibu ameidokeza DIRAMAKINI Blog. 

Kifo chake kinaelezwa kimetokea mkoani Morogoro baada ya kuugua ghafla.

Baragaza alikuwa mahiri katika vipindi mbalimbali ikiwemo Je? Huu ni Uungwana ikiwemo Mambo Mambo na RFA,pamoja na Asili ya Mtanzania kupitia Star Tv.

Taarifa zaidi DIRAMAKINI Blog itaendelea kukuletea hapa, Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema. Amen

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news