Watu wenye ulemavu waishukuru Serikali kwa kuleta chanjo ya Corona nchini

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

IKIWA bado zoezi la utoaji chanjo ya Virusi vya Corona (COVID-19) likiendelea hapa nchini,baadhi ya watu wenye walemavu mkoani Dodoma nao wamekuwa miongoni waliofika katika vituo vilioainishwa kwa ajili ya kupatiwa huduma huku wakiishukuru Serikali kwa kuleta chanjo hizo.
Akizungumza na DIRAMAKINI BLOG Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Wilaya ya Dodoma Mjini (SHIVYAWATA), Dekariswa Mmari mara baada ya kupatiwa chanjo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma amesema kuwa, watu wenye walemavu Wilaya ya Dodoma Mjini zoezi la chanjo wamelipokea kwa mikono miwili.

Aidha, amesema kuwa kama walemavu wana Kila sababu ya kupata chanjo ya COVID-19 ili kuweka miili yao kwenye kinga, kwani kutokana na changamoto walizonazo wapo kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa magonjwa mbalimbali ikiwepo Covid-19.

"Kwa niaba ya watu wenye walemavu wenzangu hapa Dodoma Mjini tunaishuru Serikali yetu kwa kuleta chanjo hizi pia mkuu wetu wa mkoa Mheshimiwa Anthony Mtaka kwa kutupa kipaumbele wakati wa zoezi zima la kupata chanjo. Sisi watu wenye walemavu tumepata fursa ya kuchanjwa na tumepata huduma nzuri, japo awali tuliogopa sana kutokana na habari za kwenye mitandao ya kijamii wengi walidai endapo wakipata hizo chanjo wangepoteza maisha yao.

"Lakini sisi kama viongozi bado tuna kazi kubwa ya kuendelea kutoa elimu kwa wenzetu walemavu ambao bado wana wasiwasi juu ya chanjo hiyo ya CORONA huku tukiwaeleza faida watakazopata pale watakapojikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kuwapata na wiki ijayo tumepanga kuwaandaa wengine baadhi kwa ajili ya kwenda kupatiwa chanjo,"amesema Mmari.

Nae Mulesi Manyama ambaye ni Mlemavu wa miguu kutoka jijini Dodoma amesema, katika kipindi hiki cha janga la Corona ambacho dunia inapitia ni muhimu kuhakikisha kila mtu anachukua hatua zote za kujikinga ili kuhakikisha afya inakuwa salama.

"Kwa muktadha huu nimeamua kuchanja ili kupata kinga ya kupambana na huu ugonjwa ikitokea nimeambukizwa hivyo ni vyema kila mmoja wetu kuhakikisha kwa namna yoyote ile anajikinga na kuwa na afya njema,"amesema Mnyama.

Pia amewataka walemavu wasiogope chanjo dhidi ya maradhi kwani zimekuwepo na watu wamekuwa tukichanja, bali wajaribu kufuata ushauri wa madaktari na kila mtu anawajibu wa kulinda afya yake mwenyewe.

Na ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Afya iendelee kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa chanjo ili fikra mbaya zilizojengeka ziweze kuisha.

Kwa upande wake Evance Thadeo ni mmoja wa walemavu amesema kuwa, kitendo cha Serikali kuleta chanjo hizo ni nafuu kwao kwani hakuna gharama zozote wanazodaiwa tofauti na muda tu.

Amesema, elimu iendelee kutolewa kupitia vyombo vya habari ili kuondoa hofu kwa baadhi ambao wanahofia usalama wao huku akiwasihi wahudumu wa afya kutumia lugha nzuri kwa walemavu na wanaofika kupatiwa chanjo ya COVID-19 jambo ambalo litazidi kuhamasisha wengine.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa Daktari Best Magoma akizungumzia hali ya utoaji chanjo unavyoendelea Mkoa wa Dodoma amesema kuwa, wananchi wa rika zote wamekuwa na mwitikio mkubwa jambo ambalo linaonyesha elimu imewafikia.

"Licha ya Serikali kuweka kipaumbele kwa makundi matatu ya afya ,wazee na wa magonjwa sugu ila Kuna hadi vijana ambao wanakuja kuomba ili nao wapatiwe chanjo tunaona ni kiasi gani wengi wamechangamkia fursa ya chanjo, kwani kwa kituo kimoja kuna wanaweza kuchanja watu zaidi ya 300 kwa hapa mjini,"amesema.

Hata hivyo amesema walemavu nao wamekuwa mstari wa mbele kuja kupatiwa Chanjo ya COVID-19 japo Bado hakujawa na utaratibu wa kuweka takwimu zao binafsi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news