Waziri Mwigulu atia saini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kieletroniki za Kutuma na Kutoa Fedha za Mwaka 2021


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipokea marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kielektroniki za Kutuma na Kutoa Fedha kwa Mwaka 2021 kwa ajili ya kusaini kutoka kwa Afisa Sheria Mwandamizi wa Wizara hiyo, Bi. Mwantum Sultani, marekebisho hayo yamepunguza viwango vya tozo za miamala hiyo kwa asilimia 30, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisaini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kielektroniki za Kutuma na Kutoa Fedha kwa Mwaka 2021, marekebisho hayo yamepunguza viwango vya tozo za miamala hiyo kwa asilimia 30, jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, akiteta jambo na Afisa Sheria Mwandamizi wa Wizara hiyo, Bi. Mwantum Sultani, baada ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kusaini marekebisho ya Kanuni za Tozo za Miamala ya Kielektroniki za Kutuma na Kutoa Fedha kwa Mwaka 2021, jijini Dodoma. (Picha Na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini -WFM)

Post a Comment

0 Comments