Alhaji Muhidin Ndolanga, bosi wa zamani TFF afariki

DAR ES SALAAM, Aliyewahi kuwa Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Alhaji Muhidin Ndolanga kilichotokea leo jioni Dar es Salaam.

Ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo ameiambia Mwanaspoti kuwa kifo cha Mzee Ndolanga kimetokea katika Hospitali ya TMJ.
"Ni kweli shirikisho na familia ya mpira wa miguu tumepata pigo la kuondokewa na Mzee wetu Alhaji Muhidin Ndolanga aliyewahi kuwa Rais wa TFF kilichotokea leo katika Hospitali ya TMJ.

Kwa sasa taratibu za kuuhifadhi mwili wa Mzee wetu ndio zinaendelea hivyo taarifa rasmi kuhusu utaratibu wa mazishi zitatolewa," alisema Ndimbo.

Ndolanga atakumbukwa kwa misimamo yake pindi alipokuwa Rais wa TFF na kabla ya hapo akiwa mwenyekiti wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) kuazia 1992 hadi 2004.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news