Sita mbaroni kwa tuhuma za kuvujisha mtihani wa Darasa la Saba

MOROGORO,Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia watuhumiwa sita kwa kuhusika na njama za kuvujisha mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi uliofanyika hivi karibu.

Miongoni mwao ni pamoja na walimu watano na mlinzi mmoja waliokuwa wakisimamia mtihani katika Shule ya Msingi Kambara wilayani Mvomero.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro,SACP Fortunatus Musilimu, amesema watuhumiwa hao ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kambara, Juliana Thomas, Msimamizi Mkuu wa Mtihani Antonia Pastory, Mwalimu Doma Sekondari.

Wengine ni Mtoto Francis, Mwalimu Shule ya Msingi Kinda, Mwalimu Dorine James wa Shule ya Msingi Madizini, Mwalimu Habibu Hango na Mlinzi wa mtihani kituo hicho Mohammed Bajuka.

Kamanda Musilimu amesema, jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wengine watano kwa kupatikana na nyara za serikali yakiwemo meno matatu ya tembo yenye uzito wa kilogramu 23.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news