DC Mgandilwa atoa maagizo kwa Madiwani Jiji la Tanga

Na Hadija Bagasha, Tanga

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashimu Mgandilwa amewataka madiwani wa Halmshauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha wanasimamia vizuri fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Mgandilwa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza kwenye kikao maalumu cha baraza la madiwani cha kupitia taarifa za hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha 2020/21.

Amesema, fedha nyingi za miradi ya maendeleo zinaweza kutumiwa vibaya ikiwa madiwani watashindwa kutekeleza wajibu wao wa kuangalia thamani ya kiwango cha fedha kinachotumika.

DC Mgandilwa amesema, ni wajibu wa madiwani kuhakikisha wanasimia ipasavyo matumizi ya fedha zinazotolewa kwenye miradi inayotekelezwa kwa kuhakikisha wanasimamia kiwango cha fedha kilichotolewa na kazi husika iliyofanyika.
Katika kikao hicho Naibu Meya wa jiji hilo, Joseph Colvas amesema kuwa watahakikisha madiwani wote wanasimamia ipasavyo fedha zinazotolewa kwenye miradi lengo likiwa kuharakisha maendeleo ya wananchi kwa haraka lakini pia kusimamia vyema fedha za umma.

"Ni jukumu letu sisi madiwani tunapaswa kuwa mfano wa kuigwa na madiwani wengine katika maeneo mengine juu ya matumizi yetu katika makusanyo na hata matumizi ya fedha za miradi niwaase madiwani wenzangu tuchape kazi tuzitumie kwa malengo yaliyokusudiwa fedha zinazotolewa kwajili ya wananchi wetu, "alisisitiza Naibu Meya Colvas.

Katika kikao hicho Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba amewataka madiwani wa jiji la Tanga kujitafakari na kuhakikisha katika vikao vyao wanajadili vitu vyenye tija kwa wanachi wao.
"Mkoa wa Tanga umepata viongozi wapya,tumepata mkuu wa mkoa mpya,tumepata mkuu wa wilaya mpya na tumepata mkurugenzi wa jiji mpya nataka wasome haya mambo na wasome hawa watu wanataka nini katika kuliendesha baraza la madiwani,pamoja na kuendesha jiji la Tanga,

Aidha Mwenyekiti Mkoba amewataka madiwani hao kuhakikisha wanapitia kwa kina taarifa hiyo ya fedha waliyofikishiwa ili kuweza kuhoji pale watakapoona panahitaji kufanyiwa marekebisho.

"Niwaambie tu kuwa Mheshimiwa Rais amekuwa anapigia makelele na kusisitiza maamuzi katika vikao sasa kama tunakuja tunakaa dakika tano...dakika mbili tunasema tumemaliza inakuwa, hakuna litakalofanyika,"amesema Meja Mstaafu Mkoba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news