Rais Dkt. Mwinyi awashukuru wachungaji, maaskofu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameitaka Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi itakayobainisha maeneo yaliotengwa kwa ajili ya makaazi pamoja na yale ya ibada.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na viongozi wa Dini ya Kikristo alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar kwa ajili ya mkutano wa viongozi hao uliofanyika leo.(Picha na Ikulu). Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiteta na baadhi ya Viongozi wa Dini ya Kikristo kabla ya Mkutano wa Viongozi hao uliofanyika leo katika Ofisi ya Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Baadhi ya Masister na Viongozi wengine wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo ni miongoni mwa washiriki wa mkutano wa Viongozi hao uliofanyika leo katika Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar mgeni rasmi alikuwa rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi.(Picha na Ikulu).

Dkt. Mwinyi ametoa wito huo leo alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kikristo katika mkutano uliofanyika Kituo cha Amani Utengemano kilichopo Welezo, Mkoa Mjini Magharibi, ambao uliwahusisha Maaskofu, Wachungaji na waumini wa madhehebu mbalimbali wa dini hiyo, ukiwa na lengo la kuwashukuru wnanachi hao baada ya kumchagua kwa kishindo katika uchaguzi mkuu uliopita, sambamba na kusikiliza changamoto zinazowakabili.

Amesema kuwepo kwa mipango bora katika matumizi ya Ardhi kutaondoa changamoto zinazojitokeza za kufanyika ujenzi wa holela wa nyumba za Ibada, ambapo waumini wa dini tofauti hujenga majengo yao katika eneo moja.

Aidha, Dkt. Mwinyi amewataka watendaji wanaoshughulikia utoaji wa vibali vya kazi nchini, kuondokana na urasimu pamoja na utozaji wa gharama kubwa kwa watumishi wa Dini wanaotoka nje na kuja nchini kwa njia ya kujitolea. Baadhi ya Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.alipokuwa akizungumza na Viongozi hao katika mkutano uliofanyika leo katika Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar. (Picha na Ikulu). Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo katika mkutano uliofanyika leo katika Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar. (Picha na Ikulu). Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti a Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo katika mkutano uliofanyika leo katika Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar (Picha na Ikulu). Baadhi ya Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo wakifurahia hotuba iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.alipokuwa akizungumza na Viongozi hao katika mkutano uliofanyika leo katika Ukumbi wa Amani Utengamano Welezo Mjini Zanzibar. (Picha na Ikulu).

Mapema, akisoma Risala ya Baraza la Maaskofu Zanzibar, Mchungaji Shukuru Maloda alisema wakristo wa Zanzibar wanaounga mkono juhudi zinazochukuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na utulivu, ili kufanikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

Nae, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Zanzibar, Agostino Shao ameiomba Serikali kuweka Mawakili wa kushughulikia kesi za udhalilishaji tangu hatua za mwanzo za upelelezi wa kesi hizo, ikiwa ni hatua ya kuziba mianya kwa jamii kufanya usuluhishi au kuingiza muhali na kuvuruga mustkabali wa kesi hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news