Fei Toto aibeba Yanga SC, KMC yapigishwa kwata

NA GODFREY NNKO

Kijana kutoka visiwa vya marashi, Feisal Salum Abdallah (Fei Toto) amefanikiwa kuiwezesha Klabu ya Yanga kutwaa alama tatu.

Ni baada ya kuzichakaza nyavu ndani ya dakika 24 katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/2022.

Ushindi huo uliharibu mipango ya Kagera Sugar ambao wemefungiwa katika dimba la Kaitaba lililopo Bukoba mkoani Kagera.

Fei Toto amefunga bao hilo kwa shuti la mguu wa kushoto akimalizia mpira uliookolewa na kipa, Issa Chalamanda kufuatia shuti la awali la mshambuliaji Mkongo, Fiston Mayele Kalala.

Wakati huo huo, timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ya KMC imeanza vibaya katika mchezo wa kwanza kwa kuchapwa mabao 2-0.

Mtanange huo umepigwa katika Uwanja wa Black Rhino huko Karatu mkoani Arusha dhidi ya Polisi Tanzania.

Vitalis Mayanga mshambuliaji wa Polisi Tanzania ndiye aliyevuruga mipango ya KMC katika dakika ya tatu na la pili dakika ya thelathini.

Post a Comment

0 Comments