Mkurugenzi Mkuu mpya REA asisitiza bidii, maarifa na uadilifu kazini

Na Veronica Simba-REA

MKURUGENZI Mkuu mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Said amekabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake, Mhandisi Amos Maganga leo Septemba 29, 2021 ambapo amewaasa watumishi kufanya kazi kwa bidii, maarifa na uadilifu.
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Said (kulia) akipokea Kabrasha lenye taarifa mbalimbali kuhusu REA kutoka kwa Mtangulizi wake, Mhandisi Amos Maganga katika hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi, Dodoma, Septemba 29, 2021. (Picha na Veronica Simba-REA).

Mhandisi Said amesema, matumaini ya Watanzania, hasa wa vijijini, yanategemea dhamana ambayo REA imepewa.
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Said akizungumza na wafanyakazi wa REA baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Mtangulizi wake Mhandisi Amos Maganga, Septemba 29, 2021 Dodoma. (Picha na Veronica Simba-REA).

“Tukitetereka katika kutimiza majukumu yetu, tutafifisha matumaini ya Watanzania wengi ambao wanategemea nishati kama nyenzo ya kubadilisha maisha yao,”amesisitiza.
Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiimba wimbo wa ‘Mshikamano Daima’ wakati wa hafla fupi ya kumpokea Mkurugenzi Mkuu mpya wa REA, Mhandisi Hassan Said na kumwaga Mtangulizi wake Mhandisi Amos Maganga (hawapo pichani), Septemba 29, 2021 Dodoma. (Picha na Veronica Simba-REA).

Aidha, Mkurugenzi huyo mpya wa REA alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini kuwatumikia Watanzania katika wadhifa huo na kuahidi kuwa hatamwangusha.

Vilevile, ametoa pongezi kwa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) chini ya Mwenyekiti Wakili Julius Kalolo, Mtangulizi wake Mhandisi Maganga pamoja na wafanyakazi wote wa REA kwa kazi nzuri iliyofanyika na kufikia hatua nzuri katika kusambaza nishati vijijini.
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Said akipokea shada la maua kutoka kwa mfanyakazi wa REA, Eshimuni James, alipowasili rasmi Makao Makuu ya Ofisi hizo Dodoma, Septemba 29, 2021. (Picha na Veronica Simba-REA).

“REA ni miongoni mwa taasisi za umma ambazo zimefanya kazi kubwa sana na ambazo zimegusa maisha ya wananchi. Huwezi kupata mafanikio kama haya ikiwa hauna bodi imara na yenye weledi mkubwa, menejimenti nzuri na wafanyakazi wanaojituma,”amefafanua.

Sambamba na hayo, Mhandisi Said ameomba ushirikiano kutoka kwa bodi, menejimenti na watumishi wote wa REA katika kutekeleza majukumu yake.
Mhandisi Amos Maganga akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) – (hawapo pichani), baada ya kukabidhi rasmi Ofisi kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa REA, Mhandisi Hassan Said, Septemba 29, 2021 Dodoma. (Picha na Veronica Simba-REA).
Mapokezi ya Mkurugenzi Mkuu mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Said, alipowasili rasmi Makao Makuu ya Ofisi hizo Dodoma, Septemba 29, 2021. (Picha na Veronica Simba-REA).

Awali, akizungumza baada ya kukabidhi rasmi ofisi kwa Mkurugenzi mpya, Mtangulizi wake Mhandisi Maganga amemshukuru Mungu, Bodi na Wafanyakazi wote wa REA kwa kumpatia ushirikiano katika kipindi chote alichofanya kazi nao. (Picha na Veronica Simba-REA).
Mapokezi ya Mkurugenzi Mkuu mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Said, alipowasili rasmi Makao Makuu ya Ofisi hizo Dodoma, Septemba 29, 2021. (Picha na Veronica Simba-REA).

Mhandisi Maganga amebainisha kuwa, mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya nishati vijijini, yanatokana na ushirikiano mkubwa alioupata kutoka kwao.

Amewataka kumpatia ushirikiano wa aina hiyo, Mkurugenzi mpya huku akibainisha kuwa yeye binafsi anamwamini na anamtambua kama mchapakazi na mwenye uhodari katika utendaji kazi.

Akizungumza kwa niaba ya bodi, Mwenyekiti Wakili Julius Kalolo amempongeza Mhandisi Hassan kwa kuaminiwa na Rais na kuteuliwa kushika wadhifa huo mkubwa. Amemwahidi kuwa Bodi itampatia ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo (kulia), akimtambulisha rasmi Mkurugenzi Mkuu mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Said kwa Wafanyakazi wa REA mara baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi, Septemba 29, 2021 Dodoma. (Picha na Veronica Simba-REA).

Vilevile, amempongeza na kumshukuru Mhandisi Maganga kwa ushirikiano alioutoa kwa bodi katika kipindi chote alichofanya kazi katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu. (Picha na Veronica Simba-REA).
Kaimu Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Elineema Mkumbo akimkaribisha (kwa niaba ya Menejimenti) Mkurugenzi Mkuu mpya wa REA Mhandisi Hassan Said (kushoto) alipowasili rasmi Makao Makuu ya Ofisi hizo Dodoma, Septemba 29, 2021. (Picha na Veronica Simba-REA).

Aidha, wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa niaba ya Menejimenti ya REA na wafanyakazi wote, Kaimu Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti, Mhandisi Elineema Mkumbo, Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Grace Sengula pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) Tawi la REA, Swalehe Kibwana, wameahidi ushirikiano pamoja na kutekeleza yale yote aliyoyasisitiza Mkurugenzi mpya.

Mhandisi Hassan Said aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa REA kuanzia Septemba 23, mwaka huu akitokea Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) alikokuwa akifanya kazi kama Meneja Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu mpya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Said (wa tatu-kulia) na Mtangulizi wake, Mhandisi Amos Maganga (wa tatu-kushoto) baada ya makabidhiano rasmi ya ofisi leo Septemba 29, 2021 jijini Dodoma. Wengine pichani ni baadhi ya Wajumbe wa Bodi. (Picha na Veronica Simba-REA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news