Haji Manara awalaani Rivers FC,wafinywa kimya kimya

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

"Tumefanyiwa mambo ya kihuni na tumepewa matokeo ya Corona dakika 45 kabla ya mchezo huu ni uhuni;

Afisa Habari wa Yanga SC, Haji Manara ameyasema hayo, wakati wawakilishi hao wa Tanzania wakizimiwa ndoto yao katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Msafara mzima wa Yanga na wadau wengine ulifanya vipimo vya Uviko 19 jana saa 11 asubuhi kama ambavyo kanuni ya mashindano ya Shirikisho la Soka Afrika CAF inavyoelekeza.

Wawakilishi hao wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa mbio zao zimehitimishwa nchini Nigeria.

Yanga ilikuwa na kazi ya kusaka ushindi wa zaidi ya bao 1-0 kwa kuwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Leo pia ugenini nchini Nigeria Yanga imepoteza kwa kufungwa bao 1-0, hivyo wametolewa kwa jumla ya mabao 2-0.

Ni katika mechi ya marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Adokiye Amiesimaka mjini Port Harcourt, Nigeria.

Post a Comment

0 Comments