Hotuba ya Rais Samia UNGA76 yaingia kwenye 10 bora ya hotuba muhimu Duniani

NA MWANDISHI MAALUM

Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wa Tanzania aliyoitoa Septemba 23, 2021 kwenye Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA76) huko New York nchini Marekani imetajwa kuwa miongoni mwa hotuba saba muhimu zaidi kwenye kikao hicho.Soma hotuba yote hapa>>>
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha kumbukumbu katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Jijini New York Marekani, baada ya kuhutubia mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo Septemba 23,2021. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Hotuba ya Rais Samia imechaguliwa na tovuti ya Marekani ‘Foreign Policy (FP)’ miongoni mwa hotuba muhimu zaidi kutolewa kwenye kikao hicho na pia ni ya pekee kutoka kwa mkuu wa nchi mwanamke.

Rais Samia amekuwa mmoja wa wakuu wachache wa nchi wanawake kutoka Afrika kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 

Viongozi wengine ambao hotuba zao zimeelezea mambo muhimu ni pamoja na Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Marekani Joe Biden, Rais wa Brazil Jair Bolsonaro, Rais wa Lebanon Michel Aoun, Rais wa Iran Ebrahim Raisi na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.

Katika chapisho lao ‘FP’ liliwataka wachangiaji na waandishi wa kurasa zao kupima hotuba wanazoona zina uzito mkubwa au zina mambo muhimu zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news