James Rugemalira aachiwa huru

KISUTU, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia mashtaka na kumwachia huru mfanyabiashara maarufu Tanzania, James Rugemalira.

Hatua hiyo inatokana na Mkurugenzi wa Mashataka nchini (DPP) kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya mshtakiwa huyo.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuachiwa leo Septemba 16, 2021, Mike Ngalo ambae ni wanasheria wa Rugemalira amesema mteja wake amefutiwa mashtaka yote baada ya DPP kusema kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.
 
Juni 2017, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini Tanzania (TAKUKURU ) iliwafikisha Mahakamani Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth na Rugemalira kwa makosa sita ya uhujumu uchumi ikiwemo kosa la kuisababishia serikali hasara.

Post a Comment

0 Comments